MTANGAZAJI wa Clouds FM ambaye pia ni mmiliki wa tovuti ya
www.shaffihdauda.com ameingia matatani baada ya kudaiwa kuweka nyaraka
za siri za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwenye mtandao wake.
TFF imemtaka Shafiih Dauda kutoa maelezo kuhusiana na barua ya
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) aliyoiweka kwenye
mtandao wake huo huku akijua kwamba barua hiyo ilikuwa ni siri.
Barua
hiyo ambayo TFF walitumiwa na FIFA kuelezea hatua za kuchukuliwa
kutokana na kusimamishwa kwa mchakato wa uchaguzi wa TFF baada ya
baadhi ya wagombea kuulalamika, FIFA baadaye ilitoa maelekezo kuhusu
mchakato huo kwa barua ambayo ilituma kwa Rais wa TFF, Leodegar Tenga.
Rais
wa TFF katika mkutano wake na waandishi wa habari ambao Dauda
alihudhuria alibainisha kuwa barua hiyo ya FIFA hawezi kupewa kila mtu,
na kuruhusu waandishi kuisoma kwa Ofisa Habari wa TFF bila kuondoka
nayo.
Wakati Rais Tenga anazungumza na waandishi wa habari (Mei 2
mwaka huu), nakala ya barua hiyo ya FIFA ilikuwa kwa viongozi wakuu wa
TFF pekee, na viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo. Hivyo TFF imemtaka Dauda kutoa maelezo ya mahali alipoipata
barua hiyo ndani ya siku saba.
No comments:
Post a Comment