WAKATI Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe akiendelea kuziba masikio yake bila kujali maneno ya Mtangazaji wa Clouds Fm Loveness Love maarufu kama DIVA, amedhihirisha wazi ni kiasi gani amezama kwenye penzi la msanii wa kiwango cha juu nchini Kenya Prezzo kwa kummwagia sifa kemkem kupitia mitandao ya kijamii.
Mwanadada huyo ambaye awali alikuwa anatoka na Mbunge wa kigoma Kaskazini Zitto Kambwe alimwagia sifa kemkem mpenzi wake wa sasa ambaye ni mwanamuziki maarufu nchini Kenye kuwa ndiye mwanaume pekee aliyemfanya awe na furaha ambayo hakuwahi kuipata kwa mpenzi wake wa zamani kwa mara ya kwanza.
Diva aliandika hayo katika mtandao wa Blackberry Messenger(BBM) kuwa anajisikia furaha kumbwaga mpenzi wake wa zamani baada ya kukutana na mwanamuziki maarufu nchini Kenya na mshindi wa pili kwenye shinadano la Big Brother Africa (BBA).
Diva ambaye ni Mtangazaji wa kipindi cha Mapenzi (alaza roho) cha clouds Fm alitangaza wazi baada ya kuzama kwenye penzi la Prezzo kuwa yeye ni ni zaidi ya wasichana wote walioshirirki Big Brother Africa ni zaidi ya wasichana wote wa Kenya nani zaidi ya wasichana wote wa Africa mbele ya Prezzo
Mara tu baada ya kumwagia sifa nyingi mpenzi wake wa sasa Prezzo, Diva alimgeukia mpenzi wake wa zamani Zitto Kabwe na kumtweet kibuti Zitto Kabwe katika ukurasa wake wa Tweeter. Akimchana Rais huyo mtarajiwa Diva alisema, Zitto hufikiri kwamba maelezo (Tweets) zako zimechelewa? fikiri kwa undani kuhusu unachokieleza na ujue cha kufanya. "Zitto Kabwe usijaribu kumsukuma mtu aliyefikia mwisho, kuwa makini kwa kumsukuma mtu aliyechoka na ujue kitakachoweza kutokea,Zitto Kabwe zingatia sana unapomsukuma mmtu aliyefikia mwisho ujue kwamba anaweza akalipuka muda wote na unaweza kununua dharau kwa bei rahisi, Zitto Kabwe unajua binadamu akichoka kinachofuata anaacha kuongea na kuchukua hatua ya kuongea kwa sauti ya juu zaidi ya matendo na anaacha kuongea na kutekeleza kwa vitendo"alisema Diva katika ukurasa wake wa Tweeter. hii ndiyo sehemu ya mwisho ya makala ya machungu ya mitandao ya kijamii kwa Mh. Kabwe
No comments:
Post a Comment