Dar es Salaam,Tanzania
MATUSI ya Rais wa Rwanda Paul Kagame kwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jakaya Mrisho Kikwete yamewagawa Watanzania.
Rais Kagame alimtukana Rais Kiwete kwa kuita ushauri wake kwamba ni ushauri wa kijinga kwa wanyarandwa,awali Rais Kikwete alizishauri nchi za Rwanda na Congo DRC kukutana na kumaliza tofauti zao kwa njia ya amani.
Rais Kikwete alitoa ushauri huo wakati wa mkutano wa kujadili amani na mpango wa ulinzi nchini Congo DRC uliofanyika katika Makao Makuu ya AU mjini Addis Ababa Ethiopia.
Katika ushauri huo Rais Kikwete alisema kwamba ni vyema Rais Kagame akakaa katika meza ya mazungumzo ya amani na Rais wa Congo DRC Joseph Kabila ili kumaliza tofauti zao badala ya kutumia nguvu ya kijeshi.
“Nimekaa kimya kwa kipindi kirefu na kwa jinsi nilivyoweza kwa sababu nilifikiri kwamba mazungumzo ya kipuuzi yaliyozungumzwa na watu wajinga yamemalizika "alisema Rais Kagame.
Katika hatua nyingine Rai Kagame alisema kwamba ushauri huo wa Rais Kikwete ni sawa na kuwachezea wanyarandwa mbele ya mataifa. Rais Kagame aliyasema hayo katika sherehe ya kuhitimu mafunzo ya maofisa wa jeshi wapatao 45 katika kituo cha mafunzo ya kijeshi siku ya Juma Tatu nchini Rwanda.
Ingawa haijajulikana mara moja kwamba baadhi ya watu walioandika maoni yao katika mtandao wa Facebook ni watanzania ama baadhi yao si watanzania, huku wakidai kwamba Rais Kagame yuko sahihi
Kikwete yuko sahihi kwa mantiki ya kumaliza suala hilo kwa muda mrefu. Hao wanaoitwa wana FDRL kwa muda mrefu wako Mashariki mwa Kongo wanaua, wanabaka, na kila mara wanataka kurudi Rwanda kwa amani au kwa fujo!Je,tuwaache tu wafanye hayo kwa sababu hawaifanyii Rwanda?Najua yanayomuuma Kagame kwa sasa!asimuingizie JK wetu.Kagame tuachie shida zetu hapa kama kwenu mko safi kaa kimya!
ReplyDelete