Tuesday, 11 June 2013

Obama, Xi wamalizana


Rais Barack Obama  wa Marekani (kushoto) akiwa na  Rais wa China ,  Xi Jinping baada ya kumaliza mkutano wao wa kwanza kati ya China na Marekani, nchini China. 

China. Barack Obama na Xi Jinping wamemaliza mkutano wao wa kwanza kati ya China na Marekani, wakiweka hali ya kuelewana na kukubaliana kuhusu sera na kupata jawabu kuhusu Korea ya Kaskazini, hali ya hewa na mtandani.
Marais hao walitumia saa nane pamoja katika muda wa siku mbili, katika makundi ya yaliyokuwa na ukaribu ya wafanyakazi, katika chakula cha jioni, pamoja na kutembea katika bustani nzuri katika eneo lililotunzwa vizuri katika Jangwa la Califonia.
Ulikuwa mkutano wa kwanza kati ya China na Marekani tangu Xi mwenye umri wa miaka 59 kuchukua madaraka kamili ya nchi hiyo Machi na Obama mbunifu wa kupanga upya diplomasia ya Marekani kuelekea Bara la Asia ambaye anatazamwa kwa jicho la shaka na China, kuchukua madaraka katika kipindi cha pili cha utawala wake.
Pande zote mbili zilitaka kulegeza mazungumzo hayo kati ya China na Marekani kuwa ya kawaida, na hali hiyo imeonekana kufanikiwa.
 Katika wakati fulani Obama na Xi, wakitafuta msimamo wa pamoja kama wanasiasa, walitayarisha mitazamo yao katika kuelekeza kule ambako wanataka kuyaelekeza mataifa yao.
Wakati Xi alipoondoka maofisa wa Marekani walisema , viongozi hao wawili walizungumza moja kwa moja kuhusu maeneo ya matatizo, usalama katika mtandao, wakashutumu kukwama  kuhusu mpango wa kinyuklia wa Korea ya kaskazini na kukubaliana kuhusu msukumo mpya wa pamoja kuhusu mabadiliko ya tabia nchi.

No comments:

Post a Comment