Friday, 14 June 2013

Walala hoi wote kuuza simu zao,kurudia barua za mkononi


Pamela Mollel ni kati ya watumiaji wakubwa wa simu za kiganjani,wataokumbwa na tozo za asilimia 14.5 kwa ajili ya kuchangia garama za elimu nchini Tanzania
WAKATI hali ya maisha ikizidi kupanda kila kukicha,Serikali imepanga kuwatoza watumiaji wa simu za mkononi ili kupata fedha za kugarimia elimu.Wamiliki wa siku za mkononi nchini Tanzania watatozwa asilimia 14.5.
Akizungumza Bungeni jana Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa alisema kwamba tozo hiyo itakuwa chanzo kipya cha mapato ya Serikali, Dk Mgimwa alisema Serikali inakusudia kutoza gharama hizo kwa watumiaji wa simu zote za mkononi kuanzia mwezi ujao ikiwa ni pamoja na kutoza ushuru wa bidhaa zote za kiwango hicho kwenye huduma zote za simu za kiganjani, badala ya muda wa maongezi peke yake.
“Katika ushuru huu, asilimia 2.5 zitatumika kugharimia elimu hapa nchini... Hatua hii imezingatia mapendekezo ya Kamati Maalumu ya Spika ya Kushauri kuhusu mapato na matumizi ya Serikali,” alisema Dk Mgimwa.
Waandishi wa habari wakiwa Bungeni Dodoma anaripoti kwamba Kama vile haitoshi, Waziri Mgimwa alitangaza kuongeza wigo wa kutoza ushuru wa bidhaa kwenye huduma za simu za mezani (TTCL) na zisizokuwa na waya.
Pia waziri alitangaza kuanzisha kodi ya zuio ya asilimia 10 ya kamisheni (commission) ya usafirishaji wa fedha kwa njia ya simu za mkononi. Kodi hiyo itakusanywa na kampuni za simu kutoka kwa wakala wanaotoa huduma za kusafirisha fedha kupitia simu za mkononi.
Katika hatua nyingi Waziri Dk Mgimwa alisema kwamba Mapendekezo hayo ya ni utekelezaji wa ushauri wa Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali, (CAG)Ludovick Utouh.
Katika Ushauri huyo CAG aliwai kuiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), itafute vyanzo vipya vya kodi ili kuongeza mapato ya Serikali katika mwaka wa fedha wa 2013/14.
Miongoni mwa maeneo ambayo Ripoti ya CAG iliyoishia Juni 30, mwaka jana ilishauri kuangaliwa, ni pamoja na huduma za kuhamisha fedha kwa njia ya simu za kiganjani maarufu kama M-Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money na Easy Pesa.
CAG alishauri kuwa kampuni za simu kulipa kodi ya zuio ya malipo ya kamisheni inayolipwa kwa wanaofanya biashara hiyo na kodi hiyo ya zuio ipunguzwe kutoka katika kodi ya mwisho itakayotakiwa kulipwa na kampuni za simu

No comments:

Post a Comment