NAIBU
wa Rais Bw William Ruto, jana alivunja kimya chake kuhusu hatua ya
rais wa Marekani Barack Obama kutozuru humu nchini kwa kusema hatua
hiyo haina madhara yoyote kwa Kenya.
Huku akiongea
katika kanisa la Katoliki la St Gabriel Bahati, kaunti ya Nakuru, Bw
Ruto alisema nchi hii ina 'marafiki’ wengine wengi duniani ambao inaweza
kushirikiana nao huku akiongezea kuwa hatua ya rais Obama kukwepa
kutembelea Kenya haiwezi kutatiza kwa vyovyote vile uhusiano mwema
uliopo wa kibiashara baina ya Marekani na Kenya.
“Tunaiheshimu nchi ya Marekani nayo inafaa kuwaheshimu Wakenya,” akasema Bw Ruto.
Alisema
serikali tayari imeanzisha mikakati ya kuimarisha ushirikiano wa
kibiashara na mataifa mengine huku akikariri kuwa safari ya Rais
Uhuru Kenyatta nchini Uganda ambapo alikutana na rais wa nchi hiyo
Yoweri Museveni na mwenzao wa Rwanda rais Paul Kagame kujadili jinsi
nchi hizo tatu zinaweza kushirikiana kibiashara, ni miongoni mwa
mikakati hiyo.
“Nchi yetu
inamcha Mungu na kamwe hatutaruhusu mataifa ya kigeni kutuletea
tamaduni ambazo zinakinzana na desturi zetu,” akasema Bw Ruto huku
akirejelea hotuba ya Rais Obama nchini Senegal ambapo aliitaka nchi
hiyo kuheshimu haki za Mashoga.
Wakati mwafaka
No comments:
Post a Comment