YAPO
mengi mazuri ambayo huenda mpenzi wako aliwahi kukufanyia, je uliwahi
kumshukuru kwa kukufanya ufarijike? Naamini Mungu amekujaalia kuwa na
mpenzi mzuri, mwenye kila sifa ambayo ulitamani awe nayo, je ulishawahi
kumsifia hata kwa kumwambia ni mzuri?
Huenda
ulishawahi kufanya hivyo lakini kwa taarifa yako wapo ambao wanahisi
kufanya hivyo eti ni ulimbukeni. Ulimbukeni? Kumsifia mpenzi wako
unaona ni ulimbukeni wakati wataalam wa masuala ya mapenzi wanaeleza
kuwa, wanawake ni watu wanaopenda kusifiwa sana hata kwa madogo
wanayoyafanya?
Unaona
hatari gani kumsifia mpenzi wako kuwa ni mzuri? Unadhani unatumia nguvu
gani kumsifia mpenzi wako kutokana na mahaba mazito anayokupata?
Kwa taarifa yako unaweza kuona ni kitu kidogo sana lakini madhara yake kwenye penzi ni makubwa.
Kumsifia
mpenzi wako kwa yale anayokufanyia kuna faida nyingi sana lakini kwa
leo nitagusia chache. Kwanza kunaongeza mapenzi. Mume/mke anaposifiwa
kuwa anajua mapenzi hata kama si kwa kiwango kikubwa, anafarijika sana.
Unapomwambia
mpenzi wako: ‘Dear nashukuru kwa mapenzi uliyonipa jana, umenipa furaha
ya ajabu ambayo siamini kama kuna mtu mwingine wa kunipa, nakupenda
sana’.
Maneno
kama haya hutumii nguvu wala muda mwingi kuyafikisha kwa mpenzi wako
lakini uzito wake ni mkubwa. Kwanza anajihisi aliyekamilika kwa kufikia
hatua ya kufanya mambo yakamridhisha mpenzi wake na kwa mazingira hayo
anaamini huwezi kumsaliti. Hisia hizo zitamfanya azidi kukupenda.
Hilo
ni kwa wote yaani kwa mwanaume na mwanamke. Lakini pia unapomsifia
mpenzi wako kwa yale anayokufanyia, unamfanya aongeze kasi ya kukufanyia
ili nawe uzidi kumpenda.
Kwa mfano, unapokutana na mpenzi wako kisha ukamwambia ‘umependeza kweli mpenzi wangu, nazidi kukupenda kwa unavyovaa’.
Mtu
anayeambiwa maneno haya atajitahidi sana siku zote aonekane nadhifu na
wa kuvutia kwa mpenzi wake akijua kwamba, akivaa ilimradi kuvaa,
hatamfurahisha mpenzi wake. Kwa maana hiyo kumsifia mpenzi wako
kunamfanya azidi kuwa bora.
Lakini kusifia kusiwe kwa kinafiki. Usimsifie mpenzi wako eti ili kumfanya ajione bora kumbe katika uhalisia siyo hivyo.
Tusifiane
pale inapobidi huku tukijua kuwa kwa kufanya hivyo tutapata faida.
Tusiwe na tabia ya kuchukulia poa kila tunachofanyiwa na wapenzi wetu.
Kama
kakuridhisha kimapenzi, msifie kwamba yeye ni muhimu kwako kwa kuwa
amekupa ulichotarajia. Amekupikia chakula kizuri, msifie kuwa yeye ni
mpishi mzuri. Hiyo italinogesha penzi na utashangaa kila siku
inayokwenda kwa Mungu penzi lenu linachanua.
Lakini
mbali na hayo, unatakiwa kuridhika kwa kile unachokipata kutoka kwa
huyo mpenzi wako ulinaye kwa sasa. Najua kwenye uhusiano wengi tumetoka
mbali. Wapo waliowahi kuwa na wapenzi zaidi ya mmoja huko nyuma na kila
mmoja alikuwa na kiwango chake cha kukuridhisha.
Inawezekana
kuna ambaye unamkumbuka kwa mapenzi mazito aliyokuwa anakupa zaidi ya
huyo uliyenaye. Hiyo ni historia, imepita! Kama huyo uliyenaye si
mtaalam sana wa kukufikisha pale unapopata, ridhika na hicho kidogo
unachokipata endapo atakuwa anaonesha kukupenda kwa dhati.
Mpe moyo, msifiesifie kidogo kwa hiyo furaha kiduchu anayokupa huku ukiamini kuwa, atabadilika kadiri siku zinavyokwenda.
Kumbuka
cha msingi katika maisha yetu ni kumpata mtu mwenye mapenzi ya kweli na
si kumpata anayeweza kukuridhisha katika mambo kadha wa kadha
No comments:
Post a Comment