Mtoto
huyo, ambaye anaishi katika kijiji cha Changani Kivunge wilaya ya
Kaskazini ‘A’ Unguja, ameonesha maajabu, baada ya kuanza kusema akiwa na
umri wa miezi miwili, kwa kutaja majina ya Mwenyezi Mungu, Mtume
Muhammad (SAW) na maneno ya kumtukuza Mwenyezi Mungu.
Mkuu wa wilaya hiyo, Riziki Juma Simai, akizungumza na Zanzibar Leo, amethibitisha kuwepo mtoto huyo.
Alisema
mtoto huyo amefikishwa ofisi ya Mkuu wa Mkoa na familia yake baada ya
mama yake aliyefahamika kwa jina moja la Dawa, kutakiwa kuwasilisha
ujumbe alionao mtoto huyo kwa jamii.
Alisema
kabla ya kuzaliwa, mama yake alisema kuwa alikutwa na mambo ya maajabu
baada ya kujiwa na kiumbe akimueleza uwezo wa mtoto wake wakati akiwa
tumboni na kumchagulia jina la kumpa baada ya kuzaliwa.
Mkuu
wa wilaya huyo alisema, kiumbe hicho kilichokuwa katika mazingira
yasioelezeka pia kilimtabiria mama huyo kwamba atazaa mtoto wa kiume.
Pia
alimuambia baada ya mtoto huyo kuzaliwa atakuwa na mambo ya ajabu na
kumtaka kumtunza na asimuogope na baadae kiumbe hicho kiliondoka.
Alisema
baada ya tukio hilo, na siku zake za kuzaa kutimia alijifungua mtoto wa
kiume na kumpa jina la Fahazal na ndipo alipoanza kushuhudua maajabu
ikiwa ni pamoja na kuzungumza akiwa na miezi miwili.
Alisema
mtoto huyo alikuwa akitamka maneno ya kumtukuza Mwenyezi Mungu ikiwemo
Allwah, Yaraabi na kutaja jina la Mtume (SAW) huku akiwataja kwa majina
watu waliokuwemo nyumbani kwao.
Mkuu
wa wilaya hiyo alisema hivi sasa mtoto huyo, amekuwa akiwasomea dua
watu wanaofikishwa kwake kwa matatizo ambapo huonesha ishara ya kuinua
mikono juu ya kuitikia dua wakati ikisomwa.
Alisema
kwa muda mrefu, familia yake iliendelea kuishi naye, lakini mama yake
alifuatwa tena na kiumbe hicho na kumtaka kufikisha ujumbe wa mtoto huyo
mbele ya jamii akitaka jamii iombe dua kwa wingi kwani vifo vingi
vinaweza kutokea nchini.
Alisema
kiumbe hcho kilirudi baada ya mama wa mtoto huyo kupuuza ujumbe wa
mwanzo aliopewa na ndipo alipoamua kutafuta watu wa kumsaidia ambapo
walimuelekeza kufuata viongozi wa dini.
Alisema,
baada mama huyo kupokea ujumbe huo, aliamua kuutekeleza kwa kuwafuata
baadhi ya walimu katika kijiji hicho kuelezea mkasa huo, ili aweze
kupata msaada.
Viongozi
wa dini walimtaka mama huyo, kulifikisha suala hilo katika ngazi ya
serikali, kutokana uzito wake kwa jamii, ambapo walimshauri kuonana na
uongozi wa mkoa.
Mkuu
huyo wa wilaya alisema, jana asubuhi, alimpokea mama huyo akiwa na
mtoto wake pamoja na shahidi ambaye ni mkaazi wa kijiji hicho ambapo
walithibitisha maajabu ya mtoto huyo.
Alisema mtoto huyo huzungumza baadhi ya wakati na kwamba anazungumza lugha tofauti ikiwemo kiingereza, kiarabu.
Alisema
wameifikisha familia hiyo kwa Mkuu wa Mkoa ili kufanyiwa mahojiano
zaidi ambapo serikali itajua nini la kufanya hapo baadae.
Alisema
wanalazimika kulifanyia kazi suala hilo, kwa vile tayari imetolewa
tahadhari ya kutokea balaa litakalowahusisha watu wengi.
No comments:
Post a Comment