Maelezo yaliyoandikwa kwa mkono kwenye
kurasa 9 na mwanamke anayetafutwa zaidi duniani, Samantha Lewthwaite aka
‘White widow’ yameonesha jinsi alivyonuia kupandikiza mzuka wa kigaidi
kwa wanae.
Magaidi wa baadaye? Samantha Lewthwaite aliandika kuwa anawaandaa wanae, (pichani) kuja kuwa magaidi kama baba yao
Karatasi hizo, zilipatikana kwenye
nyumba aliyokuwa akiishi nchini Kenya ambapo yeye na wanakarakati
wengine wa kiislamu walikuwa wamepanga kushambulia hoteli mbili na kituo
kikubwa cha manunuzi,.
Nyumba ya Kenya ambayo Samantha anadaiwa alikuwa akiishi
Polisi pia waligundua risasi za AK-47 na
picha za watoto wanne wa mwanamke huyo. Karatasi hizo zimeonesha kuwa
anakuza watoto hao wafuate nyayo za baba yao, Germaine Lindsay
aliyejitoa mhanga na kuua watu jijini London.
Watoto wake wadogo, Abdur-Rahman mwenye miaka mitano na Surajah, 3, ni
watoto wa gaidi aliyezaliwa London, Habib Saleh Ghani. Lewthwaite
anatuhumiwa kupanga mashambulio kwenye maeneo ya Kenya yenye watalii
wengi.
Mwanamke huyo aliyebadilisha dini na
kuwa muislamu, anakisiwa pia kuhusika kwenye shambulio la mwezi uliopita
kwenye jengo la Westgate jijini Nairobi ambapo watu 67 waliuawa.
Watoto wake aliozaa na Lindsay, Abdullah, 9 na Ruqayyah, 8, wana
majina ya kati Shaheed na Shahidah.
Lewthwaite alikuwa na ujauzito Ruqayyah
kipindi Lindsay alipojilipua. Inadaiwa kuwa alikuwa amejificha nchini
Tanzania au Somalia. Kwenye maelezo hayo, mwanamke huyo anaeleza jinsi
alivyobarikiwa kuwa na mwanaume mgambo na jinsi alivyojitolea kuyaacha
maisha ya raha kupigana na wasio waislamu.
No comments:
Post a Comment