Hebu tutafakari mahusiano ya
muda mrefu au mahusiano yanayopelekea ndoa!
Kama mnapenda mapenzi yenu
yadumu hadi pale “kifo
kitakapo watenganisha”, basi ni bora kuhakikisha kwamba
mahusiano ama mapenzi yenu yamejengwa katika msingi mkuu na imara ambao
ni – URAFIKI.
URAFIKI ni msingi muhimu katika kutengeneza mahusiano imara na
yenye mafanikio. Bila urafiki hamna lolote. Mambo mengine ni ya muhimu pia katika
mahusiano, bila ya shaka, lakini
unahitaji ya ziada ili kuweza
kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika maisha ya mahusiano
ambazo hakuna mtu ambaye anaweza kuzikwepa.
Kama mtu binafsi unapaswa
kuboresha uwezo wako binafsi pale inapokuja suala la mahusiano. Badala ya
kuangalia zaidi upande wa pili wa kutafuta mshirika wa mahusiano ni vyema zaidi
ukatumia muda mwingi kutafakari ni aina gani ya mtu ambaye unatarajia kujenga
naye urafiki. Kujenga urafiki ndiyo hasa mwanzo wa mahusiano. Ni kushirikiana
zaidi kwa kufahamiana, kujuana, kufahamu malengo yenu katika maisha, thamani yenu
na yale ambayo kila mmoja wenu anayapendelea ama hapendezwi nayo. Pamoja na
mambo mengine mengi mazuri ambayo yatawafanya kuwa wapekee.
Kuna muda wa kutosha sana katika maisha ya mahusiano kwa ajili ya
mapenzi na kujitoa kwa mwenzako, hakuna haja ya kukimbilia hayo!
Ni kweli kwamba kadiri unavyo
ahirisha kujiingiza katika mapenzi na kujenga urafiki, ndivyo jinsi ambavyo
utaweza kujenga mahusiano yaliyo bora na mwenzi wako wa baadaye katika maisha.
Kwa mwenendo huo mtajifunza na kuona kama mnaendana na mko tayari kila mmoja
kwa mwenzake.
Hivyo basi kama itakuwa
hamuendani ama mmoja hayuko tayari kwa mahusiano hayo ni rahisi kuachana huku
kila mtu akiwa na utu wake kama mlivyokutana!
Kujenga msingi imara ni muhimu, mara baada ya kuujenga ni
rahisi kuendelea kutengeneza maisha na mahusiano mazuri juu ya msingi huo. Chukua
muda, fahamianeni, jengeni urafiki ambao mtaweza kuuenzi kwa muda wa miaka
mingi katika maisha yenu na hatimaye kuweza kuwa na maisha bora ya
mahusiano yenye mafanikio na faida kwa maisha ya pande zote husika.
No comments:
Post a Comment