Monday, 4 November 2013
Urembo wa Nyusi/ Shaping Your Eyebrows
Nyusi ulizonazo kabla ya kutumia wanja zitatengeneza base ya kushape na kudefine.
Mfano nyusi hizo kwenye picha mwishoni ni nyembamba zinahitaji kupunguzwa kidogo na kuzipa mkunjo kidogo.
Nyusi zianzie wapi?
Zisianze mbali na macho yako yanapoanzia, unapozipunguza uwe makini na hili.
Mkunjo/Arch ya nyusi ianzie wapi?
Mkunjo wa nyusi zako uanzie karibu na nusu ya nyusi zako kama nyuzi 90 (90 degrees) kutoka kwenye pua .Usipandishe mkunjo wa nyusi sana, haitapendeza na nyusi zitakupa muonekano tofauti kidogo.
Nyusi iishie wapi?
Nyusi isipitilize sana mwisho wa macho yako kwa mtazamo wa uhalisia zaidi (natural look).
Kunyoa nyusi mno mara nyingi inasababisha zipoteze kujaa kwake na kupungua ujazo.
Jazia sehemu ambazo hazina nyusi kwa kutumia wanja unaoendana na rangi ya nyusi zako, make-up ni kwa ajili ya kuongezea uzuri wako wa asili na si kubadilisha mwonekano wako wa uhalisi. Hakuna mwenye nyusi nyekundu, kijani au bluu jitahidi utumie wanja wa brown au mweusi unaoendana na rangi ya nyusi zako kwa kuchora kwa mbali kiasi na si kwa mgandamizo ili uvutie zaidi.
Nyusi zikitengenezwa vizuri uzuri wa macho na shape ya macho inaonekana sawia kama picha hapo juu.
Ikiwa unakutana na mtu na kitu cha kwanza unachokiona kwake ni nyusi zake, hakika zitakuwa hazipo katika shape inayotakiwa au ametumia wanja wa kupitiliza.
Till next time......
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment