Imevuja
kuwa mwanaume atakayetaka kumuoa staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth
Michael ‘Lulu’ atalazimika kutoa si chini ya shilingi laki nane
(800,000) kama mahari ili kumuoa mwigizaji huyo.
Kwa
mujibu wa chanzo makini cha gazeti hili, wanaume wengi wamekuwa
wakimendea kufunga ndoa na Lulu lakini wakashindwa njia za kumpata.
Ilidaiwa
kuwa kikwazo kikubwa wanachokutana nacho ni namna ya kumfikia na kigezo
cha dini kwa sababu Lulu hataki kuolewa na muislam kwani hayupo tayari
kubadili dini.
Akizungumza
na Amani katika mahojiano maalum, mapema wiki hii, mama wa Lulu,
Lucresia Karugila alisema kwa upande wake yupo tayari kupokea mahari
yoyote ilimradi mwanaye awe ameridhiana na mwanaume husika.
“Unajua Lulu ameshakua, mambo ya kumwingilia mtoto kwenye vitu binafsi ni ya kizamani.
“Siwezi
kupanga mahari, sijui laki nane au laki ngapi. Kiasi chochote ni sawa
cha msingi mwanangu awe amekubaliana na huyo mwanaume.
“Hajaniambia kama kuna mtu anataka kuleta mahari,” alisema mama Lulu.
Kwa
upande wake Lulu alisema: “Kwa sasa sina wazo la kuolewa ila naweza
kuamka kesho nikabadili uamuzi.” Alipoulizwa kama ni kweli atatakiwa
kulipiwa mahari ya laki nane alisita kidogo.
Kuhusu
kigezo cha dini staa huyo alikiri kuwa kati ya vitu anavyozingatia ni
hicho kwani hataki mwanaume wa kumbadilisha dini na mahari yake
itategemea na mtoaji
KWA NINI LAKI 8?
Uchunguzi
uliofanywa na gazeti hili kwa wanandoa wengi waliofunga pingu za maisha
hivi karibuni ulibaini kwamba wengi walilipa mahari ya kati ya shilingi
laki sita na milioni moja na nusu huku wastani ukiwa ni shilingi laki
nane
No comments:
Post a Comment