Tuesday 21 January 2014

Mwaka 2014 umeanza vibaya kwa kupoteza watu mashuhuri Mwigizaji 'Letti' afariki dunia

Mwigizaji maarufu, Lesego Motsepe maarufu zaidi kama Letti aliyejijengea jina kubwa kutokana na ushiriki wake katika tamthilia maarufu ya Isidingo katika kipindi cha nyuma, amefariki dunia.

Kwa mujibu wa chanzo cha taarifa, msanii huyu alikutwa na kaka yake akiwa amekwishakata roho nyumbani kwake huko Randburg Afrika Kusini.

Bado kuna taarifa mbalimbali kuhusiana na chanzo cha kifo cha mwanadada huyu ingawa taarifa kutoka katika familia yake zinasema kuwa Letti amefariki kifo cha kawaida.

Mwigizaji huyu maarufu alijitangaza hadharani kuwa anaishi na virusi vya UKIMWI mwaka 2011 na kusema kuwa ameishi kwa matumaini kwa miaka 13 na wengi wanahusisha kifo chake na ugonjwa huu hatari.

No comments:

Post a Comment