Monday, 20 January 2014

Rais Kikwete awapandisha vyeo makanali

Napenda kuwakumbusha suala na nidhamu ni jambo muhimu kwani ndiyo kioo chetu katika jeshi hivyo nasisitiza kuendelea kuzingatia jambo hilo.


Rais Jakaya Kikwete ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, amewapandisha vyeo maofisa 28 kutoka Kanali na kuwa Brigedia.

Huku Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Samweli Ndomba akiwataka maafisa hao kuchapa kazi kwa bidii ili kuongeza ufanisi wa Jeshi.
Hatua ya Rais Kikwete kuwapandisha vyeo maofisa hao imefanywa kwa mujibu wa kanuni za Majeshi ya Ulinzi inayompa mamlaka kufanya hivyo.
Wakati Rais Kikwete akiwapandisha vyeo maofisa hao, Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Samweli Ndomba kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange, amewataka kuendelea kuchapa kazi kwa bidii ili kuleta tija na maendeleo jeshi.
Pia mnadhimu huyo amewasisitizia maafisa hao kusimamia nidhamu na uwajibikaji kwa sababu ndiyo msingi wa mafanikio katika utendaji wa jeshi.
“Napenda kuwakumbusha suala na nidhamu ni jambo muhimu kwani ndiyo kioo chetu katika jeshi hivyo nasisitiza kuendelea kuzingatia jambo hilo. Lingine ambalo ningependa tuendelea kulizingatia ni kufanya kazi kwa weledi,” alisema.
Kulingana na taarifa iliyotolewa na JWTZ, maofisa waliopandishwa vyeo ni pamoja na Kanali Denis Raphael Janga, Kanali Jason Nestor Musikula, Kanali Jackson King Mrema, Kanali Martin Amos Kemwaga, Kanali Joseph Cosmas Chengelela, Kanali Martin Nikubuka Mwankanye, Kanali Harold Kidundi Mziray, Kanali Emmanuel Peter Kapesa na Kanali Mwita Wambura Isamulyo.

Wengine ni Kanali Francis Asilia Njau, Kanali Pendo Uledi Kamungwele, Kanali Moses Adolph Shinyambala, Kanali Ibrahim Abdarahamani Kimario, Kanali Michael Garo Luwongo, Kanali Nelson Hosea Msanja,Kanali Blasius KalimaMasanja, Kanali Aloyce Damian Mwanjile, Kanali Rajabu Goma Hanti na Kanali Ignas Beatus Mubofu.
Pia wamo Kanali Dominic Basil Mrope, Kanali Hamis Issa Majumba, Kanali Salehe Omari Semtaua, Kanali Henry Sweko Kamundo, Kanali Sylivester Msafiri Minja, Kanali John Bangantagoka Bishoge, Kanali Anselm Shigongo Bahati, Kanali Robinson Mboli Mwanjela na Kanali Kaisy Philip Njelekela.

No comments:

Post a Comment