Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi, amesema hoja kwamba Watanzania hawana mtaji wa kumiliki vitalu vya gesi si sahihi kwa kuwa gesi yenyewe ni mtaji wa kutosha kwa Watanzania.
Pia amewaomba viongozi wa dini wasitoe uamuzi juu
ya watu mbalimbali waliotoa maoni yao kuhusu umiliki, ushirikishwaji na
uwezeshwaji katika sekta ya gesi.
“Nawasihi wanaposhiriki kwenye mikutano ya aina
yoyote wasikilizemaoni ya pande zote mbili kabla ya kutoa maamuzi yao,
ili Mungu aweze kuwaongoza katika kutoa msimamo ambao utanufaisha
Watanzania wote kwa njia ya mapendekezo,” alisema Mengi.
Alisema kinachopiganiwa siyo sekta binafsi ama
vitalu vimilikiwe na mtu mmoja mmoja mzawa bali, vitalu vya gesi
vimilikiwe na kampuni ama vikundi vya Watanzania hasa wazawa.
Alisisitiza kuwa mtu yeyote anayesema anatakakumiliki kitalu cha gesi yeye binafsi, anasema uongo.
“Sisi tunataka vitalu vimilikiwe na makampuni ama
vikundi vya Watanzania hasa wazawa ambao watauza hisa kwa Watanzania
wote iliwapate fursa ya kushirikikatika uchumi wa gezi,” alisema.
Kwa muda sasa, kumekuwa na malumbano kati ya
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospiter Muhongo na Mwenyekiti wa
Sekta Binafsi, Mengi kuhusu Watanzania kumiliki wa vitalu vya gesi
mkoani Mtwara.
Waziri huyo aliwahi kukaririwa akisema kuwa
Watanzania wana mitaji midogo ambayo haiwaruhusu kuwekeza katika sekta
ya gesi ambayo alisema uwekezaji wa wake ni wa gharama kubwa.
Hata hivyo, Mengi kwa upande wake, amepuuza hoja
hiyo na kusisitiza kuwa Watanzania wana uwezo wa kuwekeza katika sekta
hiyo mpya katika uchumi wa nchihni. Alisema madai ya Profesa Muhongo
hayana msingi.
No comments:
Post a Comment