Wafanyakazi wa kampuni ya Swissport katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Mnyerere wakipeleka kwenye gari jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Chuo cha Dar es Salaam (UDSM), Balozi Fulgence Kazaura jana, ulipoletwa kutoka nchini India alikofariki dunia Jumamosi iliyopita.
Baada ya kuwasili kwa ndege ya Shirika la Ndege la Emirates, msafara wa waombolezaji uliokuwa na magari zaidi ya 15 ulianza safari ya kwenda Hospitali ya Hurbert Kairuki iliyopo Mikocheni ambako mwili wa marehemu umehifadhiwa.
Mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Balozi Fulgence Kazaura (74) umewasili nchini jana ukitokea Chenai, India alikokwenda kwa matibabu ya saratani.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki,
Makamu Mkuu wa Chuo cha UDSM, Profesa Rwekaza Mukandala, ndugu, jamaa na
marafiki walijitokeza Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
(JNIA) kupokea mwili wa Balozi Kazaura aliyefariki Februari 22, mwaka
huu.
Baada ya kuwasili kwa ndege ya Shirika la Ndege la
Emirates, msafara wa waombolezaji uliokuwa na magari zaidi ya 15
ulianza safari ya kwenda Hospitali ya Hurbert Kairuki iliyopo Mikocheni
ambako mwili wa marehemu umehifadhiwa. Msemaji wa familia, Charles
Mwombeki alisema leo kutafanyika shughuli za kifamilia za kuaga nyumbani
kwake, Oysterbay kuanzia saa 7:00 mchana.
Alisema baada ya kumaliza kutoa heshima za mwisho,
mwili huo utapelekwa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Peter Oysterbay
kuanzia saa 8:00 kwa Ibada ya kumwombea na baadaye utarudishwa Hospitali
ya Kairuki. Anatarajiwa kuzikwa Jumamosi mkoani Kagera.
No comments:
Post a Comment