Aliyekuwa kuwa Mawaziri Mkuu; Edward Lowassa
Kwa upande wake, Ngeleja ndiye aliyetumia muda mfupi zaidi kwani aliingia katika ukumbi wa mahojiano saa 8:10 na kutoka 8:50.
Waliowahi kuwa Mawaziri Wakuu; Edward Lowassa na Frederick Sumaye jana walifika mbele ya Kamati Ndogo ya Maadili ya CCM kutoa maelezo juu ya tuhuma za kufanya kampeni za urais kabla ya wakati.
Mbali na wastaafu hao, mwingine ambaye jana
alifika mbele ya kamati hiyo ambayo ilikuwa chini ya Makamu Mwenyekiti
wa CCM Bara, Philip Mangula na Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman
Kinana ni Waziri wa Nishati wa zamani na Mbunge wa Sengerema, William
Ngeleja.
Mjumbe mwingine wa kamati hiyo aliyehudhuria kikao
hicho kilichofanyika kwenye Ukumbi wa White House jana ni Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi.
Wajumbe wengine ni Dk Maua Daftari, Shamsi Vuai Nahodha na Pindi Chana
ambao hata hivyo, hawakuhudhuria.
Hata hivyo, wanachama wengine watatu, Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, Waziri wa Nchi
(Ofisi ya Rais Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira na Naibu wa Sayansi
na Teknolojia, January Makamba ambao wote wanatazamiwa kuitwa leo mbele
ya kamati hiyo.
Vyanzo kutoka ndani ya chama hicho vilieleza kuwa
Membe alikuwa katika ziara ya Rais Jakaya Kikwete na alitarajiwa kurejea
nchini jana jioni.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya
kukamilika kwa mahojiano ya makada hao watatu jana, Kinana alisema
shughuli ya kuwahoji wengine itaendelea leo.
“Kazi haijakwisha, kesho (leo) tunaendelea.”
Waliyosema baada ya kuhojiwa
Akiwa amevalia mavazi rasmi ya CCM, Lowassa
alihojiwa kwa takriban saa moja na nusu kwani aliingia katika kikao
hicho saa 4:56 asubuhi na kutoka saa 6:40 mchana akiwa ametumia takriban
saa moja na nusu na alitoka akiwa mwenye furaha.
Alipoulizwa kuhusu mahojiano hayo Lowassa:
“Mazungumzo yalikwenda vizuri. Yalikuwa na lengo la kujenga chama kwa
ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015,” alisema Lowassa huku akitabasamu.
Muda mfupi baada ya Lowassa kutoka, Sumaye aliingia kuanzia saa 6:46 na kutoka saa 8:05.
Baada ya kutoka, Sumaye pia hakuwa tayari
kuzungumzia kuhusu mahojiano hayo... “Tunawasubiri wakubwa watakavyotoa
jawabu.” Alipoulizwa sababu za kutumia muda mwingi katika kikao hicho
alisema: “Tulikuwa tunakunywa chai.”
Kwa upande wake, Ngeleja ndiye aliyetumia muda mfupi zaidi kwani aliingia katika ukumbi wa mahojiano saa 8:10 na kutoka 8:50.
Aliwaambia waandishi wa habari waliokuwa nje ya
ukumbi huo kuwa mazungumzo hayo yalikuwa ni ya kichama na kikazi zaidi
na kwamba hizo ni taratibu za CCM kuwaita wanachama wake kwa ajili ya
kutoa maelekezo.
Kuhusu kutangaza nia ya kugombea urais kabla ya
muda uliopangwa na chama, Ngeleja alisema wanaongozwa na kanuni na
taratibu na kwamba wakati wa kutangaza kugombea urais haujafika.
Alisema hakuitwa kuhojiwa kwa kutangaza nia ya kuwania urais kabla ya muda... “Sijatangaza, sijasema, sina ugomvi huo.”
No comments:
Post a Comment