Je, chumba chako ni kama stoo? Umejaza vitu chini ya uvungu wa kitanda? Je mara nyingi umejikuta unatafuta hata vitu vidogo tuu ambavyo pengine ulidhani unajua wapi vilipo? Basi makala hii inakuhusu.
Fikiria
umeenda ofisini kwa mtu, una haraka zako ila unahitaji mtu huyo atie saini
nyaraka yako ambayo uliiwasilisha hapo wiki moja iliyopita. Kufika hapo anachukua
dakika 20 kutafuta wapi nyaraka ipo (kwakuwa vitu vyake vimejipanga hovyo). Unamuona
wakati anatafuta nyaraka yako, anaochana nyaraka nyingi ambazo zinaonekana
hazina umuhimu tena kwa ofisi yake ila zilikuwepo tuu hapo ofisini.Baada ya kuipata
hiyo nyaraka anagundua kuwa hana kalamu.
Baada ya
kuhangaika kuitafuta kalamu hapo ofisini kwake, amekata tamaa anaamua kuenda
ofisi ya jirani kuazima. Hata hivyo huko nako anacheleweshwa kwakuwa huyo
aliyemfuata naye haioni kalamu kwa urahisi.
Ndivyo
pengine hata wewe ulivyo, una vitu vingi usivyovihitaji ila umevirundika bila
sababu ya msingi. Ok, sababu yako kuu ya msingi yaweza kuwa unatumaini
kuvitumia hapo baadae. Lakini kwa kuwa hauna taratibu ya kupitia vitu vyako
basi unajikuta umeweka vitu vingi bila msingi.
Na waweza
dhani kuwa hakuna tatizo katika kutunza vitu hivyo usivyovihitaji ila embu
kumbuka jinsi vinavyojaza chumba chako, aun yumba yako. Kuna watu vyumba vyao
vya kulala ni kama “stoo”, embu chunguza chini ya kitanda hivyo ulivyojaza
unavihitaji kweli , embu chunguza juu ya meza yako iwe ya ofisini au nyumbani
unahitaji , embu chunguza kabatini na kwenye mabegi yako, jee hivyo vitu vyote
pamoja na nguo kweli unazihitaji.
Tatizo la
kujaza vitu vingi visivyo na umuhimu kwako
ni KUPUNGUZA UFANISI wako kwakuwa utajikuta muda mwingi unatumia kutafuta vitu
vya umuhimu kwa kuwa vimesongwa na hivyo visivyo vya umuhimu.
Kupunguza
vitu visivyo na umuhimu haitoshi, jitahidi pia kupangilia vema vitu
vyako.
Kumbuka kwanini mara nyingi unajisaidia haja kubwa au ndogo ? ni kwa
sababu hata mwili wako
unahitaji kuondoa yale yasiyohitajika mwilini, ili uendelee kuwa mwenye
afya. Ndivyo na wewe unahitaji kupunguza hayo yanayokuzunguka ili uwe
mfanisi zaidi.
No comments:
Post a Comment