Thursday, 27 February 2014

Mambo 12 muhimu ya kujikumbusha kila mara upatapo majaribu katika maisha, ukianguka katika maisha au kushindwa kufikia malengo yako uliyojiwekea

Mambo 12 muhimu ya kujikumbusha kila mara upatapo majaribu katika maisha,  ukianguka katika maisha au kushindwa kufikia malengo yako uliyojiwekea


1. Usiogope. Mambo
yatarudi
na kuwa sawa tena hivyo jitahidi kuepuka hali ya kujishusha, kujilinganisha na wenzio na mwishowe kukaribisha msongamano wa mawazo (stress)

2. Hakuna mafanikio pasipo na changamoto au kushindwa hivyo tumia muda wako kujisahihisha na kujipanga upya

3. Kufikiri kwa ushindi hutengeneza nafasi za mafanikio mazuri baadae hivyo utumie muda huu kuyajadili maisha yako kwa uangalia zaidi nguvu zako kuliko mapungufu ambayo waweza kuyakabili

4. Kumbuka mafanikio huwa jirani na wewe tofauti na unavyofikiria hivyo anza kujiandaa kwa kufanikiwa upya na kuyakabili mapungufu ya mwanzo

5. Wewe sio makosa yako hivyo usijiumize sana. Wengi huamini wao nao ni matunda ya makosa yaliyo wafanya washindwe. Lakini wanasahau kuwa mambo hutokea kwa bahaati mbaya.

6. Mafunzo mema katika maisha hutujia nyakati tusizozitarajia, kumbuka katika maisha hatuna madarasa zaidi ya nyakati kama hivi ambapo twapata nafasi ya kuyaona na kuyasahihisha kwa ufasaa makosa yetu.

7. Kushindwa sio jambo baya la kukufanya ukate tamaa na kukosa nguvu za kusimama tena hivyo jipe ujasiri wa kukabiliana na changamoto zijazo

8. Kukosa unachokitaka pia huwa ni baraka kwani Mungu anajua kwa nini umekikosa wakatu huu, hivyo tegemea uwepo wa Mungu na kuzidi kuomba

9. Una kila nguvu ya kujitengenezea furaha yako mwenyewe na mafanikio mwenyewe bila kumtegemeq mtu
10. Kushindwa katika maisha ni njia ya kujifunza kwa vitendo namna ya kufanikiwa tena au kuyanyoosha mpito yako.

11. Unajitahidi hivyo ongeza bidii katika kujinasua katika hiyo hali

12. Pamoja na kushindwa kumbuka maisha yanaendelea.
Pia kumbuka una kila nafasi ya kuyafanya maisha yako kuwa bora kwa kila hali utakayoipitia kama utajitahidi kujipa nafasi ya faraja kujibidiisha, kutoumia moyoni na kuona kama umeshindwa huku ukimshirikisha Mungu wako

No comments:

Post a Comment