Friday 7 February 2014

MBUNGE LEMA AJISALIMISHA POLISI

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amejisalimisha Polisi jijini hapa, ingawa amesema hawezi kuhojiwa kwa kuwa wakili wake hayupo. Lema alisema hayo leo jijini hapa wakati akitoka Kituo Kikuu cha Polisi .


Alisema hakukamatwa, isipokuwa amekwenda mwenyewe.

"Nimejileta mwenyewe, maana nilikuwa sijui kama natafutwa, ila nimesema siwezi kutoa maelezo yangu kwa sababu wakili wangu hayupo, hivyo ni ngumu kwangu mimi kutoa maelezo yoyote, ila CCM wanadai tumefanya vurugu pale maeneo ya Kibo, ila mimi sikumbuki hizo vurugu zilipotokea'' alisema.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alithibitisha Lema kujisalimisha jana Polisi.

Alisema alichohojiwa ni suala la upelelezi. Awali, Lema na wanachama wengine watatu, wanatuhumiwa wiki iliyopita kufanya vurugu kwenye mikutano ya kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Sombetini.

Uchaguzi huo mdogo utafanyika Jumapili Februari 9, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment