Ni kichekesho cha karne kwamba akili za wajumbe wengi, badala ya kuelekezwa kwenye ufanisi wa shughuli za Bunge hilo kama kudai wapewe makabrasha yenye nyaraka zilizoandaliwa vizuri au nakala za kutosha za Rasimu ya Mabadiliko ya Katiba pamoja na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, zimeelekezwa kwenye fedha na kuchumia matumbo yao.
Kilele cha vioja na vitimbi hivyo ni pale wajumbe wengi walipozusha zogo mithili ya watoto wa chekechea kwa madai kwamba posho ya Sh300,000 wanazopewa kila siku hazitoshi na badala yake wanataka wapewe Sh420,000.
Hata kabla ya kupita wiki moja tangu
Bunge Maalumu la Katiba kuanza rasmi shughuli zake, wajumbe wake
wameendelea na vituko kiasi cha kutupa wasiwasi kama kweli wengi wa
wajumbe hao wanastahili kutuwakilisha katika chombo hicho kufanya kazi
ya kihistoria ya kutunga Katiba Mpya. Tulisema jana kupitia safu hii
kwamba wengi wa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba hawaonyeshi kama
kweli wanatambua nafasi na hadhi waliyonayo kama wawakilishi wetu katika
chombo hicho, kwani vitendo na kauli zao vinajenga picha tofauti. Ndiyo
maana tulionya kwamba Bunge linapoanza shughuli zake kwa kutawaliwa na
vioja na vituko haliwezi kamwe kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Ni jambo la kusikitisha kuwa, pamoja na angalizo
letu kwa wajumbe wa Bunge hilo, jana na juzi tulishuhudia mwendelezo wa
vitendo vya aibu ambavyo kwa vyovyote vile siyo tu vimekidhalilisha
chombo hicho, bali pia vimeibua maswali mengi miongoni mwa wananchi
ambao wamehoji kama kweli Bunge hilo limeundwa na watu wenye sifa na
hadhi ya kuitwa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba. Kilele cha vioja na
vitimbi hivyo ni pale wajumbe wengi walipozusha zogo mithili ya watoto
wa chekechea kwa madai kwamba posho ya Sh300,000 wanazopewa kila siku
hazitoshi na badala yake wanataka wapewe Sh420,000.
Ni kichekesho cha karne kwamba akili za wajumbe
wengi, badala ya kuelekezwa kwenye ufanisi wa shughuli za Bunge hilo
kama kudai wapewe makabrasha yenye nyaraka zilizoandaliwa vizuri au
nakala za kutosha za Rasimu ya Mabadiliko ya Katiba pamoja na Sheria ya
Mabadiliko ya Katiba, zimeelekezwa kwenye fedha na kuchumia matumbo yao.
Tayari wamesahau kwamba waliteuliwa kuingia katika Bunge hilo kujitolea
na kujitoa mhanga ili kuhakikisha inapatikana Katiba Mpya na siyo
kugeuza uwakilishi wao katika Bunge hilo kuwa ajira.
Kichekesho kingine ni kwamba madai hayo ya kipuuzi
waliyatoa wakati wa semina waliyoandaliwa kwa ajili ya kupatiwa rasimu
ya Kanuni zitakazoongoza shughuli za Bunge. Badala ya kuzungumzia rasimu
hiyo, wajumbe walilifanya suala la posho kuwa kipaumbele chao na kutaka
walipwe viwango vya posho kama makamishna wa Tume ya Mabadiliko ya
Katiba walivyolipwa, huku wakipuuza ukweli kwamba makamishna hao na
madereva wao walistahili kulipwa viwango hivyo kwa sababu walisafiri
nchi nzima, tena katika mazingira magumu na kufanya kazi usiku na
mchana. Uzoefu wetu umetuonyesha kwamba wengi wa wajumbe wa Bunge hili
watatumia muda mwingi kuchapa usingizi au kukacha vikao. Ndiyo maana
wanataka walipwe posho hata wasipohudhuria vikao.
Kwa sababu ya woga usiokuwa na msingi wowote,
uongozi wa Bunge umesikiliza upuuzi huo na kuteua kamati ya watu sita
eti kwenda kuona ugumu wa maisha ulivyo mitaani. Badala ya kusimamia
ukweli kwamba Sh300,000 ni nyingi sana kwa matumizi ya kila siku,
uongozi wa Bunge na Serikali sasa utakuwa unaandaa mkakati wa kuongeza
posho hizo. Hii ni kinyume na hali ya uchumi wa nchi yetu ilivyo, kwani
Serikali imeelemewa na Deni la Taifa la zaidi ya Sh27 trilioni, kwa
maana ya Sh20.23 likiwa deni la nje na Sh6.81 trilioni likiwa deni la
ndani ambalo Serikali imeshindwa kulilipa. Tusisahau kwamba ukarabati wa
Ukumbi wa Bunge umegharimu zaidi ya Sh8 bilioni.
No comments:
Post a Comment