Katika tukio la juzi, Padri wa Kanisa Katoliki,
Otto Myer (70) ambaye ni raia wa Italia, alikutwa akiwa amefariki saa
tano usiku chumbani mwake kwenye nyumba ya kulala wageni ya the
Consolata huko Westlands, Nairobi.
Mwili wa padri huyo ulipatikana kwenye chumba
hicho kando yake kukiwa na dawa, na baadhi ya jirani zake walisema
alikuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mfupi.
Juzi, Mkuu wa Polisi Jimbo la Nairobi, Benson
Kibue alisema maofisa wake wanachukulia kifo chake kuwa cha ghafla, hasa
kutokana na kwamba amekuwa akiugua kwa siku kadhaa.
“Hatutaharakisha kusema kilichomuua. Kwa sasa
tunajua hiki ni kifo cha ghafla, ikizingatiwa kuwa amekuwa akiugua.
Upasuaji wa maiti ndio utakaoeleza zaidi kilichomfanya afariki,” akasema
Kibue.
Lakini maofisa wa polisi waliofika mahali hapo
pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa gesti hiyo ambao hawakutaka kutajwa,
walisema kwamba chumbani alimokufa padri huyo mlikuwa na dawa pamoja na
pombe.
Wakizungumza na waandishi wetu, walisema kwamba
padri huyo alikuwa ameenda katika hospitali ya karibu kutafuta tiba siku
ya Jumanne.
Mwingine afia kwa hawara
Kifo cha Padri Myer kilitokea saa chache baada ya
kifo cha mchungaji Geoffrey Maingi wa Kanisa la Redeemed Gospel nyumbani
kwa mmoja wa washirika wake katika Mtaa wa Buruburu, Nairobi.
Sawa na Padri Myer, Kasisi Maingi pia alikuwa na
umri wa miaka 70 na pia alifariki dunia kwenye vyumba katika hali ya
kutatanisha.
Kwenye kisa cha Buruburu, Kasisi Maingi
alisemekana kuegesha gari lake nje ya duka la jumla la Tuskys na kwenda
nyumbani kwa mwanamke mshirika wa Kanisa lake, ambaye alikiri kuwa mbali
na kuwa kiongozi wake wa kiroho, yeye pia alikuwa rafiki yake.
Mwanamke huyo alisema kuwa mchungaji huyo alikuwa
nyumbani kwake kwa maombi. Tukio hilo lilishuhudiwa katika mtaa wa
Buruburu mjini Nairobi Kenya.
Mwili wa Maingi, ulikutwa ndani ya chumba cha mwanamke huyo, baada ya kufariki kutokana na sababu ambazo hazijulikani.
Mwili wa Maingi, ulikutwa ndani ya chumba cha mwanamke huyo, baada ya kufariki kutokana na sababu ambazo hazijulikani.
No comments:
Post a Comment