Walevi nchini Kenya wamekuwa wakilalamika kuhusu
matumizi ya kifaa malum cha kupima kiwango cha pombe walichokunywa
madereva wa usiku wanapokuwa wakiendesha magari wakiwa walevi.
Na pia sio lazima uweke mdomo wako kwenye kifaa bali unapuliza tu na kinachukua vipimo.
Usalama barabarani
Usalama barabarani umekuwa tatizo kuu nchini Kenya ambapo takriban watu elfu tatu hufa kutokana na ajali za barabarani kila mwaka .Idara ya trafiki imesema kuwa asilimia 85 ya ajali hizo husabishwa na makosa ya kibinadamu yanayochangiwa kakubwa na ulevi kupindukia.
Kumekuwa na mjadala mkali nchini Kenya ikiwa kifaa cha AlcoBlow ni salama au la kutokana na watu zaidi ya mmoja kukitumia wakati polisi wanapofanya ukaguzi wao katika vizuizi vya barabarani
Ujanja wa walevi
Josephat Baraza ni meneja wa baa moja jijini Nairobi, anasema kuwa wakati operesheni ya kurejesha usalama barabarani ni muhimu, imeleta hasa kwa wauza mpombe na wanaomiliki mikahawa.Lakini wamekuwa wajanja nao kwani wamezindua huduma ya kuajiri madereva wanaoendesha magari ya wateja wa baa yao na kuwarejesha nyumbani kwa njia salama baada ya kunywa pombe na kuendesha magari yo huku wakijozolea balaa.
Walevi wamejaribu juu chini kujinasua kutoka katika mtego wa polisi wanaoshika doria barabarani. mitandao wa jamii kama Facebook na Twitter kuonya wenzao kutopitia bara bara waliko polisi.
Licha ya hayo, Charles Keitany ambaye ni afisa mkuu anayesimamia usalama wa barabara kuu za Kenya anasema lazima wataendela na operesheni ya kuwanasa madereva walevi.
Si mara ya kwanza polisi wa Kenya kutumia kifaa vya kupima kiwango cha ulevi, kila mara hatua hii imepata pingamizi kali kutoka kwa umma ambao wamepeleka kesi mahakamani kutaka kifaa hicho kutohalalishwa.
Mahakama moja jijini Nairobi ilitupilia mbali kesi hiyo.
Kawa sasa kuna Wakenya ambao wananunua kifaa hicho kwa matumizi yao binafsi lakini mkuu wa polisi anyesimima barabra kuu za Kenya anashauri unaponunua kifaa cha kibinafsi lazima upate cheti cha kudhibitisha uhalali wake kutoka kwa shirika la kitaifa linalodhibiti ubora wa bidhaa.
No comments:
Post a Comment