Imebainika kwamba, iwapo warsha na makongamano yanayofanyika mbali yakitumiwa vyema na watu walio single na wanaotafuta wenza wa kufunga nao ndoa husaidia kufanikisha jambo hilo.
Kwanza, makongamano hukutanisha wadau mbalimbali wa rika tofauti tofauti
walio single na wasio single ambapo kwa walio single wanaweza kutumia
nafasi hiyo kusafisha nyota na kuvuta mpenzi mpya wa maisha.
Pili, kwa kawaida makongamano na warsha hukutanisha wadau wa kada
mbalimbali ambao hujadili mada zinazoendana na taaluma au utashi wa
waalikwa, hivyo ule muda wa mapumziko au majadiliano yanayofanyika kwa
makundi huwawezesha wadau kujuana na vile vile kuzungumza lugha
inayofanana kwa kuwa wote wana utashi unaofanana
Tatu, licha ya kwamba, makongamano na warsha huwa na mijadala mbalimbali
na mafunzo, lakini pia katika ratiba kunaweza kuwa na shughuli
mbalimbali kama vile ziara za pamoja kuona vivutio vya mji, sherehe za
vinjwaji (Cocktails Party) au Chakula maalum cha usiku ambapo wadau
hupata muda muafaka wa kujuana na kuzungumza kwa ukaribu jambo ambalo
linaweza kutumiwa na wadau walio single kujaribu bahati zao na hata
kupeana anuani kwa ajili ya mawasiliano huko mbeleni……
Hivyo basi kwa wale wanaotafuta wenza na walio katika nafasi nzuri ya
kupata mialiko ya kuhudhuria makongamano na warsha zinazofanyika nje ya
miji wanayoishi wanaweza kutumia hiyo fursa kujichanganya na kutumia
mbinu ya mvuto ili kumvuta mpenzi mpya wa maisha na siyo kufanya ngono
kwa ajili ya kujistarehesha, kwani hilo linaweza kuwakimbiza wapenzi
wapya walio na nia ya kuoa au kuolewa kuwa mbali na wewe kwa kukuona
kicheche…
No comments:
Post a Comment