Hebu fikiria mwanaume anatoka kazini na anapofika nyumbani tu anakutana na ‘kiama’ cha
maneno na lawama au kero. Baada ya madhila ya kazi ya kutwa nzima ya
kutafuta riziki kwa ajili ya familia, mwanaume hupenda kuona akirudi
nyumbani anapata fursa ya kupumua na kusahau adha za kazini.
Lakini anaporejea na kukutana na adha nyingine, kimaumbile hukereka.
Kimaumbile binadamu awaye yeyote anapokereka au kutishika atafanya jambo
moja kati ya haya mawili. Ama atapambana au kukimbia. Ukiona Simba na
kutishika kwa mfano, utaamua kupambana naye au kukimbia.
Kama mwanaume ataamua kupambana na hali hiyo, ni afadhali kwa sababu
inaweza kuwa ni kubishana au kupigana (mara nyingi mwanamke kupigwa)
Lakini mwanaume anapoamua njia ya pili ya kukimbia maana yake ni
kutafuta mahali ambapo akitoka kazini ataachwa apumzike kabla hajaanza
kuzogomwa na mahali hapo si pengine bali kutafuta nyumba ndogo
itakayompa nafasi ya kupumzika baada ya madhila ya kazini.
Kuna wanawake ambao wanaamini kwamba, wakisema au kulalamikia jambo mara
nyingi, yaani kila dakika, basi jambo hilo litatafutiwa ufumbuzi. Huu
ni uongo na imani ya hatari sana. Wanawake wengi ni wazungumzaji sana,
yaani wanapenda kulikuza jambo tena na tena na tena. Ni kama vile
wanajaribu kuingiza maaarifa fulani kwenye kichwa cha mtoto asiyeelewa
kirahisi.
Badala ya kuzungumza jambo kwa kifupi na upendo, hata kama ni la kukera,
mwanamke ataanza hotuba na kuhubiri kusikoisha. Badala ya kuangalia
upande mzuri wa jambo hilo na kuzungumzia upande huo ili taaarifa ifike
vizuri zaidi, mwanamke atatafuta udhaifu na kung’ang’ania kuzungumzia
upande huohuo.
Wasichojua wanawake hawa ni kwamba, miongoni mwa mambo ambayo wanaume
huyachukia ni kuhubiriwa kama vile wamekuwa wasiojua kitu na wasioelewa
kitu. Lakini pia kuambiwa jambo mara nyingi kama kwamba wao ni mbumbumbu
huwakera sana wanaume kuliko wanawake wanavyofikiria. Tabia hiyo
humfanya mwanaume amwone mkewe kama kisirani na kuanza kumkwepa au
kumdharau.
Mwanamke anaposema jambo anatakiwa kusema ni jambo gani hasa analenga,
siyo kuzunguka. Anachotakiwa ni kuzungumzia jambo hilo na kutoa nafasi
kwa mume kutafakari na kulitolea ufafanuzi au kutekeleza, siyo
kukumbushia na ya mwaka juzi. Pia si vyema kukebehi au kumkejeli mume
wakati wa kukumbushia jambo. Hii ni kwa sababu wanaume hawataki
kukumbushwa ya juzi na wala hawako tayari kuvumilia kukejeliwa……….
No comments:
Post a Comment