Saturday, 22 February 2014

Watu wa jinsia moja kuchunguzwa, Uganda.

Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni amesema kuwa anataka kuwapa fursa wanasayansi kuchunguza iwapo hisia za watu wa jinsia moja husababishwa na maumbile ama tabia kabla ya kuamua kuutia sahihi au la mswada tata wa watu wa jinsia moja.


Mswada huo uliowasilishwa bungeni mnamo mwaka 2009 awali ulipendekeza hukumu ya kifo kwa watu wa jinsia hiyo,lakini badala yake ukafanyiwa marekebisho ya kuhudumia kifungo cha jela kwa watakaopatikana na hatia.

Marekani imeonya kuwa uhusiano kati yake na Uganda utaharibika iwapo rais Museveni atatia sahihi mswada huo.

Rais Museveni amesema kuwa wanasayansi nchini Uganda watafanya utafiti huku akiwataka wanasayansi wa marekani kusaidia katika uchunguzi huo.

Waandishi wanasema rais huyo anajaribu kuwafurahisha watu wenye misimamo ya kadri mbali na kutoharibu uhusiano wake na mataifa ya magharibi ambayo ni wafadhili wakubwa wa taifa hilo.

 
waandamanaji wanaounga mkono haki za watu wa jinsia moja nchini Uganda.

No comments:

Post a Comment