MJAMZITO
wa miezi saba Bi. Mwanaidi Athumani mkazi wa Chamwino Morogoro hivi
karibuni alifanya mchepuko wa kutoka nje ya ndoa na kujikuta akijifungua
mtoto wa kiume ndani ya gesti iliyopo maeneo ya Mafisa mjini hapa,
Risasi Mchanganyiko lina data za kutosha.
Bi. Mwanaidi Athumani akiwa na kichanga chake baada ya kujifungua gesti.
Habari
zinasema kuwa mwanamke huyo alifanya mchepuko huo baada ya mumewe
kusafiri kwenda kutafuta fedha za maandalizi ya kujifungua kwake.
Bila
ya kujali kama ana mimba ya miezi saba, Mwanaidi aliingia katika gesti
moja (jina tunalo) akiwa na mwanaume anayedaiwa kufanya kazi ya kupiga
debe katika stendi ya Msamvu na mambo yalipomwendea kombo, mwanaume huyo
akatimua mbio.
Kwa
mujibu wa shuhuda wetu, Mwanaidi na mpiga debe wake walipanga katika
chumba namba 3 na baada ya kufanya mambo yao, Mwanaidi akaanza kupiga
kelele kutokana na kushikwa na uchungu. Ilimbidi mhudumu wa gesti hiyo,
Bi. Moshi Eliya afike kumsaidia Mwanaidi aweze kujifungua salama pamoja
na kwamba hakuwa na ‘gloves’ wala kitu chochote cha kulinda afya yake.
Mtoto wa Bi. Mwanaidi Athumani.
Chanzo
chetu ambacho nacho kilikuwa ni mpangaji ndani ya gesti hiyo kilisema
kuwa tukio hilo lilitokea saa 8 usiku na Mwanaidi alipiga kelele huku
akizozana na mpiga debe wake.
Kiliposikia tukio hilo, chanzo hicho
kikapiga simu kwa paparazi wetu aliyetinga katika nyumba hiyo ya wageni
kwa ajili ya kushuhudia tukio hilo.
Baada
ya kujifungua salama, paparazi wetu alimuuliza Mwanaidi kilichotokea
ndipo mwanamke huyo akafunguka kuwa alikuwa amechepuka nje ya ndoa baada
ya kukumbwa na shetani.
“Nina mume na tuna watoto watatu huyu ni wanne,
mume wangu amesafari kwa ajili ya kutafuta fedha za maandalizi ya ujuo
wa mwanetu akijua nina mimba ya miezi saba,”
alisema mwanaidi. Pamoja na
kutaka kugoma, lakini mwandishi wetu alimchukua mwanamke huyo na
kichanga chake na kuwapeleka Hospitali ya Mkoa wa Morogoro ambako
wamelazwa kwa uchunguzi zaidi.
Mhudumu
wa gesti hiyo, Bi. Moshi Eliya ambaye alikuwa mkunga wa Mwanaidi
alisema kuwa alishindwa kutumia ‘gloves’ wakati wa kumzalisha mzazi huyo
kwa kuwa alikumkuta mtoto ameshaanza kutoka. “Mtoto aliashaanza kutoka,
hata hivyo kwa usiku ule tungepata wapi hizo gloves?” alihoji.
No comments:
Post a Comment