Mawasiliano kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter
barani Afrika mwishoni mwa mwaka 2013, yaliongezeka hasa kutokana na
kifo cha hayati Nelson Mandela.
Katika ripoti hiyo, nyingi ya mawasiliano kwenye Twitter yalitokea Afrika miezi ya mwisho tatu mwaka jana.
Je ni miji ipi ambako mawasiliano kwenye Twitter yako juu? Na je mawasiliano haya yako kwenye lugha gani?
Utafiti huo iligundua kuwa mwishoni mwa mwaka 2013:
- Johannesburg ndio mji unaotwit zaidi Afrika iukiwa na maeneo zaidi la laki tatu ambako Twitter inatumika mjini humo , ukifuatiwa na Ekurhuleni maeneo (264,172) na Cairo (227,509). Miji ya Durban na Alexandria inashikilia nafasi ya nne na tano mtawalia.
- Nairobi ndio mji wenye shughuli nyingi zaidi kwenye Twitter katika kanda ya Afrika Mashariki ambapo kulingana na utafiti huo watumiaji wa Twitter wako katika maeneo (123,078), lakini ni ya sita barani Afrika ambako Twitter inatumika zaidi.
- Mji wa Accra ndio wenye mawasiliano mengi zaidi kanda ya Afrika Magharibi. Inashikilia nafasi ya nane Afrika Nzima.
- Lugha zinazotumika zaidi kwenye Twitter ni pamoja na Kiingreza, Kifaransa na Kiarabu. Lakini lugha nyingine za Zulu, Kiswahili, Afrikaans, Xhosa na Kireno ndizo zinatumika zaidi barani Afrika
- .
- Siku ambazo Twitter huwa na shughuli nyingi wakijishughilisha ni Jumanne na Alhamisi.
Allan anasema kuwa kuna mabadiliko makubwa katika matumizi ya Twitter leo ikilinganishwa na miaka miwili iliyopita.
Na bila shaka kulingana na Allan, hii inatoa nafasi nyingi zaidi na changamoto kwa makampuni, mashirika na serikali kote Afrika.
Mark Flanagan, mfumo wa Digital wa Portland anasema kuwa watumiaji wa Twitter Barani Afrika wanachangia mageuzi katika lugha pamoja na maswala ya kijamii na kisiasa.
No comments:
Post a Comment