MWALIMU Mkuu wa Shule ya Msingi
Rutamba, Wilaya ya Lindi amekutwa akiwa na nguo za ndani pekee katika
usingizi mzito kwenye kibao cha shule hiyo huku akiwa hajitambui kwa
madai ya kilichomkutana kinahusishwa na imani za kishirikina.
Tukio hilo limetokea juzi usiku baada ya mkazi
mmoja wa kijiji hicho, Juma Mbilemoto kumkuta mwalimu huyo akiwa kwenye
kibao hicho wakati alipokuwa anamsindikiza nduguye,Aisha Mbilimoto
aliyekuwa anasafiri kuelekea Dar es Salaam.
Akizungumzia
tukio hilo, shuhuda huyo alisema alimkuta mwalimu huyo akiwa amelala
chini ya kibao cha shule akiwa na nguo ya ndani tu (chupi)huku akikoroma
kutokana na kuwa na usingizi mzito.
Alisema awali hakumtambua mtu huyo
lakini baada ya kumkaribia alimtambua kuwa alikuwa mwalimu mkuu wa shule
hiyo na ndipo alipochukua jukumu la kumwamsha ili amvalishe kanga,
lakini aliikataa na kuondoka kwenda nyumbani kwake akiwa kama
alivyokutwa
Kwa
upande wao walimu wa shule hiyo walisema kuwa, wamekosa molari wa
kufanya kazi kutokana na kitendo alichofanyiwa mwalimu mwenzao.
Akizungumza kwa niaba ya walimu wenzake mwalimu wa taaluma wa shule hiyo, Francis Milanzi
alisema walimu shuleni hapo wamekosa amani na kuwasababishia kuzihama
nyumba zao kwa muda na badala yake kwenda kukesha kwenye ofisi za
walimu tangu tukio hilo litokee.
Ofisa
elimu wa Wilaya ya Lindi, Cosmas Magigi alisema amepokea taarifa za
tukio hilo kwa huzuni na amewaomba walimu kuwa na subira wakati
utaratibu wanalishughulikia suala hilo.
Magigi
aliongeza kuwa ofisi yake itafanya utaratibu wakumhamisha mwalimu huyo
na kumtafutia shule nyingine huku akiwataka wakazi wa eneo hilo kujenga
ushirikiano na watumishi ili waweze kutekeleza majukumu yao.
Hili
ni tukio la pili kutokea katika halmashauri hiyo mwaka huu ambapo la
kwanza lilitokea April katika Shule ya Sekondari Ruhokwe, mwalimu wa
shule hiyo alilazwa kwenye kibao cha shule akiwa uchi wa mnyama.
No comments:
Post a Comment