Thursday, 13 March 2014

JANGA LA MADAWA YA KULEVYA LAIKERA DUNIA

Mawaziri kutoka maeneo mbalimbali duniani wanakutana katika makao ya umoja wa mataifa mjini Vienna kuzungumzia njia za kupambana na dawa za kulevya.


Tume ya kimatifa inayoshugulikia dawa za kulevya inatarajiwa kutoa taarifa ya pamoja.
Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwepo mabadiliko muhimu kuhusu udhibiti wa dawa za kulevya duniani.

Mwezi Disemba Uruguay ikawa nchi ya kwanza kuhalalisha bangi, na baadaye majimbo ya Marekani ya Washington na Colorado yakafuata. Baadhi ya nchi za Amerika ya kusini zimetangaza kuwa vita dhidi ya dawa za kulevya vimefeli.

Lakini Baadhi ya nchi zinatoa wito kuwepo sera mpya zitakazozingatia afya ya umma na kuzuia matumizi mabaya ya dawa za kulevya.

Kuna pia baadhi ya nchi kama Iran Pakistan na Uchina ambazo zinataka kuwepo adhabu kali kwa wanaofanya biashara ya dawa za kulevya ikiwemo hukumu ya kifo.

Mkutano wa Vienna unatarajiwa kutoa taarifa ya pamoja lakini ni wazi kuwa kumeibuka tofauti.

No comments:

Post a Comment