Ukuaji wa ubongo wa mtoto wa kiume na wa kike ni tofauti sana. Msichana akili yake huanza kukua kumzidi wa mvulana ndani ya miezi mitatu ya mwanzo tangu kuzaliwa. Katika uchunguzi wa wazazi watagundua kwamba pindi wanapolea mtoto wa kike husogea haraka zaidi kuliko wakati wa kulea mtoto wa kiume,” anasema Tuzie.
Licha ya watoto wengi wa kike shuleni kutofanya vizuri katika baadhi ya masomo kama watoto wa kiume, wanasayansi wanasema mtoto wa kike hupata uelewa zaidi mapema kuliko wa kiume.
Imekuwa ni dhana ya muda mrefu miongoni mwa wanajamii katika
Afrika kuwa msichana hawezi kuolewa na mwanamume waliyelingana umri
kwa kuwa ni vigumu kuelewana na kuheshimiana.
Dhana hiyo inajikita katika kuchambua tofauti ya
ufahamu kati ya mwanamke na mwanamume wenye umri sawa. Mwanamke huwa na
akili iliyokomaa zaidi kuliko mwanamume wa umri huo huo. Utafiti mpya
umeipa uzito nadharia yao, baada ya kugundua kuwa ubongo wa msichana
hukomaa haraka kuliko wa mvulana.
Watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Newcastle wamasema
hii inaweza kusaidia kuelezea sababu za wasichana wadogo kuonekana kukua
kwa kasi zaidi, kuliko wenzao wa kiume wenye umri sawa.
Wanasayansi walitumia kipimo maalumu kwa ajili ya
kuchunguza ubongo kwa watu 121 waliokuwa na umri kuanzia miaka minne
hadi 40. Matokeo ya utafiti huu yalionyesha kwamba mchakato wa kubalehe
huanza kati ya miaka 10 kwa msichana, huku mvulana huchukua muda mrefu
kuanzia miaka 11 mpaka 20.
Dk. Marcus Kaiser, ambaye nbi mtafiti, anasema: “Hii ni sehemu ya mchakato wa kawaida wa kujifunza ubongo kwa jumla.
“Kwa kawaida hata katika utambuzi, imeonekana
kwamba msichana ana uwezo wa kushika mambo mengi zaidi kuliko mvulana,
ndiyo maana katika nchi za Afrika mtoto wa kike anapika, anajaribu
kutekeleza majukumu ya nyumbani kama mama yake, bado shuleni atafanya
vizuri, lakini si kwa mvulana. Akishazongwa na mambo mengi hupunguza
morali shuleni.”
Dk. Kaiser anafafanua kuwa hatua za ukuaji wa
mtoto wa kike ni za haraka ukilinganisha na wa kiume. Hii inatokana na
mfumo wa kike. Binti hukua haraka kutokana na homoni zake mwilini na pia
akishabalehe ndipo anakuwa na uelewa mpana kutokana na via vyake vya
mwili kumruhusu kubeba ujauzito.”
Wataalamu nchini
Tuzie Edwin, ambaye ni msemaji wa Afya ya Mama na
Mtoto kutoka Kituo cha Huduma ya Ushauri Nasaha, Lishe na Afya
(COUNSENUTH), anasema mtoto wa kike huanza kupevuka kiakili ndani ya
miezi mitatu baada ya kuzaliwa.
“Ukuaji wa ubongo wa mtoto wa kiume na wa kike ni
tofauti sana. Akili ya Msichana huanza kukua kumzidi wa mvulana ndani ya
miezi mitatu ya mwanzo tangu kuzaliwa. Katika uchunguzi wa wazazi
watagundua kwamba wakati wanapomlea mtoto wa kike, huongea haraka zaidi
kuliko wakati wa kulea mtoto wa kiume,” anasema Tuzie na kuongeza:
“Msichana hutambaa na kutembea haraka zaidi
ukilinganisha na mvulana, hata katika kuongea. Pia huwa na uelewa mpana
wa mazingira, anakuwa mwepesi kuanza kutumia choo mapema na ana
kumbukumbu kwamba hivi sasa anahitaji kujisaidia na pia huanza
kujitegemea ndani ya miaka miwili ikilinganisha na wa kiume,” anasema
Edwin.
Anasema msichana huwa mwepesi katika kuwasiliana
na pia huweza kuanza kushirikishwa katika baadhi ya mambo, kama kutumwa
dukani mapema zaidi ukilinganisha na mvulana.
“Msichana pia anawahi kupevuka ukilinganisha na mvulana, lakini
akishabalehe tu ubongo wake hukomaa haraka na hapo ndipo maumbile yake
yanapoanza kujitengeneza mapema kwa ajili ya mwili kujitayarisha kubeba
ujauzito wakati wowote. Hata hivyo akili yake hukua kwa nafasi kubwa
kipindi hiki, ukilinganisha na mwanamume ambaye ni hadi miaka 10
baadaye,” anasema Edwin.
Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi katika Taasisi ya
Chakula na Lishe Tanzania, Dk. Elifatio Towo anasema mtoto yeyote ana
uwezo wa kukua kwa haraka zaidi, kutokana na namna mzazi anavyomlisha na
haina tofauti na jinsi yake.
“Ikumbukwe kwamba mtoto yeyote anaweza kukua kwa haraka zaidi ikiwa mzazi atampa lishe bora na matunzo mazuri.
Kunyonyesha ndiyo sababu pekee inayowafanya watoto
akili zao zikue kwa haraka zaidi. Lakini ikumbukwe kwamba watoto wa
kike huwa na busara zaidi katika baadhi ya mambo na katika kufanya
uamuzi ikilinganishwa na wa kiume,” anasema na kuongeza:
“Huyu anaweza kufikiria makubwa zaidi ya umri
alionao, lakini mara nyingi inatokana na maumbile kwamba yeye ni
mwanamke hivyo kupevuka na anakuwa tayari kubeba ujauzito, mwili wake
unajitengeneza wenyewe,” anasema Dk. Towo.
Wasemavyo wazazi
Maimuna Jitegemee, mama mwenye watoto watatu,
anasema “Binti yangu niliweza kumwachia nyumba akiwa na umri wa miaka 13
tu, niliweza kusafiri na kurudi. Hata hivyo hali imekuwa tofauti kwa
mtoto wangu wa kiume, kwani licha ya kwamba dada yake yupo chuoni hivi
sasa, siwezi kumwachia nyumba japokuwa ana umri wa miaka 15.”
No comments:
Post a Comment