Tuesday, 21 May 2013

Askari magereza mmoja atuhumiwa kulawiti raia..

Alisema siku ya tukio, askari huyo alikwenda katika nyumba hiyo akiwa amempakia kijana mmoja katika pikipiki yake na kabla ya kukabidhiwa funguo ya chumba namba mhudumu wa nyumba hiyo alimweleza kuwa masharti ya nyumba yao hayaruhusu watu wa jinsia mmoja kukaa chumba kimoja.


Alikutwa katika nyumba ya kulala wageni  akiwa na kijana mmoja wa kiume ambaye inasemekana alimlawiti
Morogoro. Askari Magereza mwenye cheo cha koplo amenusurika kupigwa na  wananchi wenye hasira, kufuatia tuhuma kwamba  amewalawiti kwa siku moja vijana wawili wa kiume wenye umri wa kati ya miaka 18 na 20.
Tukio la kuwalawiti vijana hao linadaiwa kufanyika kati ya saa 7.00 mchana  na saa 2.00 usiku katika moja ya nyumba za kulala wageni iliyoko katika Mtaa wa Mafisa, mjini Morogoro.
Akisimulia mkasa huo, Meneja wa nyumba hiyo alisema ni desturi kwa  askari huyo kwenda na vijana wa kiume katika nyumba hiyo hali iliyowatia wasiwasi wahudumu.
Alisema siku ya tukio, askari huyo alikwenda katika nyumba hiyo akiwa amempakia kijana mmoja katika pikipiki yake na kabla ya kukabidhiwa funguo ya chumba namba mhudumu wa nyumba hiyo alimweleza kuwa masharti ya nyumba yao hayaruhusu watu wa jinsia mmoja kukaa chumba kimoja. Alisema askari huyo alimtambulisha kijana aliyekwenda naye kuwa ni mdogo wake na kwamba walikuwa na mazungumzo muhimu.
Lakini baada ya watu hao kuingia chumbani, mmoja wa wahudumu alipita karibu na mlango wa chumba hicho na kusikia sauti ya mahaba, hali iliyomtia wasiwasi na kulazimika kuripoti tukio hilo kwa meneja wake.
Majira ya saa 11.00 jioni askari huyo alitoka na kijana huyo na kuahidi kurudi tena baadaye na aliporudi majira ya saa 1.00 usiku alirudi na kijana mwingine anayedaiwa kuwa mwenyeji wa Mkoa wa Tanga.
Askari huyo alingia chumbani akiwa na kijana huyo na muda mfupi alitoka na kwenda dukani kununua kondomu na mafuta ya mgando pasipokujua kuwa kulikuwa na watu waliokuwa wakifuatilia nyendo zake.
Aliporudi na kuingia chumbani baadhi ya vijana waliokuwa wameandaliwa walizunguka nyuma ya chumba hicho na kuchungulia dirishani na ndipo walipojionea mambo yote yaliyokuwa yakiendelea chumbani humo.
Majira ya saa 2.00 usiku baada ya mambo hayo kumalizika kijana huyo alitoka na kumuacha askari huyo akioga. Hata hivyo kabla hajafika mbali meneja wa nyumba hiyo ya kulala wageni akiwa na wakazi wengine wa mtaa huo walionyesha kukerwa na kitendo kile walimvamia kijana huyo wakitaka kumhoji sababu za kushiriki kitendo cha aibu.

No comments:

Post a Comment