Wanawake wanaochelewa kuzaa wanakabiliwa na tisho la
kupata matatizo ya afya ya uzazi. Huu sio utafititi tu balo maoni ya
daktari mmoja mkuu mjini Nairobi Kenya.
Mtaalamu wa afya ya uzazi mjini Nairobi, Daktari John Ong'ech aliyehojiwa kuhusu hoja hii alinukuliwa akisema kuwa ''wanawake kwanza wanataka kusoma masomo ambayo hayaishi, daima wako madarasani na ofisini na kuahirisha kuzaa mtoto wao wa kwanza hii ni hatari kubwa.''
Bwana Ong'ech alisema kuwa wanaochelewesha kuzaa, wanaweza kupata Fibriods au uvimbe katika kizazi, na hata kupata magonjwa kama Saratani ya kizazi au HIV.
Fibroids zinasababishwa na kuzagaa kwa homoni mwilini, kutokana na kutumia mbinu moja ya kupanga uzazi kwa mda mrefu.
Wanaochelewa kuzaa pia wanakabiliwa na tisho la kuzaa kwa njia ya upasuaji au Caesarean .
Hatari hizi ni nyingi tu, sasa chaguo ni kwako.
Mbali na kazi kwa nini wanawake wengi wanachelewa kuzaa?Tupia maono yako hapo chini...
No comments:
Post a Comment