Friday, 7 March 2014

RAHA YA MAPENZI BWANA'' KAMA HUNA HESHIMA KWA MWEZI WAKO DAIMA HUTAONA UTAMU WA MAPENZI KAMWE


Kama huna heshima kwa mwenzi wako, daima hutaona utamu wa mapenzi. 

Katika kukamilisha makala haya, leo nakuchambulia baadhi ya hasara ambazo unaweza kukumbana nazo ikiwa hutakuwa na maelewano mazuri na mwenzi wako kutokana na kushindwa kumheshimu.

UTAKOSA AMANI
Misongo (stresses)  ya kimaisha inatesa. Inawezekana unafanya kazi sana. Wakati mwingine masuala ya kiofisi au biashara hayaendi kama inavyotakiwa. Unashinda siku nzima ukipigana kuhakikisha unaendelea mbele. Iwe umeajiriwa, umejiajiri au umeajiri! Kichwa hakitulii mpaka unahisi ni kizito.

Kufikia hapo, bila…
 
Kama huna heshima kwa mwenzi wako, daima hutaona utamu wa mapenzi. Hili nimelifafanua kwa takriban wiki tatu.

Katika kukamilisha makala haya, leo nakuchambulia baadhi ya hasara ambazo unaweza kukumbana nazo ikiwa hutakuwa na maelewano mazuri na mwenzi wako kutokana na kushindwa kumheshimu. 

UTAKOSA AMANI 
Misongo (stresses)  ya kimaisha inatesa. Inawezekana unafanya kazi sana. Wakati mwingine masuala ya kiofisi au biashara hayaendi kama inavyotakiwa. Unashinda siku nzima ukipigana kuhakikisha unaendelea mbele. Iwe umeajiriwa, umejiajiri au umeajiri! Kichwa hakitulii mpaka unahisi ni kizito.

Kufikia hapo, bila shaka unahitaji faraja. Ni kipindi ambacho unahitaji mwenzi sahihi ili aweze kukusahaulisha matatizo ya kimaisha. Mtu ambaye anakujua ulivyo, kwa hiyo inamuwia rahisi kutambua kwamba upo kwenye matatizo na kuchukua hatua zinazofaa kurekebisha hali. 
Fikiria kwamba ukiwa katika hali hiyo, unarudi nyumbani ambako unakutana na moto mwingine. Amani hakuna! Kichwa chako kinaweza kuchanganyikiwa. Kama sivyo, maradhi ya moyo yatakunyemelea. Kupata kilicho bora, kiandae. Palilia shamba na ulilime kama unataka kuvuna. 

Ukifanikiwa kumuweka mwenzi wako katika hali ya furaha, utapata faraja muda wote. Yakikufika, ukirejea nyumbani utakuta amani. Utakutana na tiba ya msongo wa mawazo ulionao. Hiyo ndiyo tafsiri ya upendo, kwa hiyo usije kukosa utulivu wa moyo. Anza leo kumfurahisha ili naye akupe mahaba tele! 

UTACHOKWA HARAKA 
Hakuna kitu kibaya kwenye mapenzi kama mtu kuchokwa na mwenzi wake. Lakini hilo siyo zito, ni rahisi mno kama hutoamua kushughulikia kasoro ulizonazo. 
Huna ubunifu, mwenzi wako haoni kitu chochote kipya. Mwenzi wako hana furaha wewe hujishughulishi. Ataanza kukuona ni mzigo na mwisho atakuchoka. Usikubali hali hiyo ikutokee, anza leo! Maisha ya kimapenzi ni mazuri sana endapo utaamua.

MTASHINDWA KUJADILIANA 
Mwenzi wako hana furaha, wewe unaingia mlango huu naye anapitia ule. Hayo ni maisha mabaya mno! Mnapatwa na mambo ambayo mngependa kushauriana, lakini mnashindwa kufanya hivyo kwa sababu mnaishi kama Simba na Yanga.

Kuna watu wanaishi kwa kalamu, wanalala mzungu wa nne! Kama matumizi, yanawekwa mezani, akitaka kutoa agizo anaandika ‘kimemo’ na kukiacha juu ya stuli! Hawaguswi kutafuta furaha yao, hawataki kuzungumza na kumaliza tofauti zao. 
Matokeo yake ni siri za ndani kuzagaa mitaani. Hili likikufika ni sawa na msiba. Chukua hatua!

HUTAPATA HUDUMA BORA 
Mwenzi wako anahitaji kuwa na furaha ili aweze kukupa huduma bora. Amini kwamba mwenzi wako ndiye anayeweza kukufanya hii dunia uione yote ni yako. Changamka leo!

Unahitaji huduma bora kutoka kwa mwenzi wako, na hilo anaweza kulitimiza endapo atakuwa na furaha dhidi yako. Hii inamaanisha kuwa, kuanzia sasa, punguza maudhi kwa mwenzi wako na umzidishie amani. Akupende na amini ndani ya nafsi yake kwamba wewe ndiye mtu bora zaidi maishani mwake. 

Ukimfurahisha, atakupa huduma bora ambayo huwezi kuipata popote. Bila shaka atakapokuhudumia, nawe utajiona umepata mwenzi sahihi wa maisha.

No comments:

Post a Comment