Friday, 7 March 2014

KUOA SIO JAMBO DOGO KAMA UNAVYODHANI, INAHITAJI KUJIPANGA KWELI KWELI.

Hivi jamani, mnazijua gharama anazoingia bwana harusi hadi anapooa? Katika hali ya kawaida kabisa, kama wewe ni mwanaume na unataka kuoa, jiandae kwa mambo haya: (hizi ni gharama utakazoingia nje ya michango ya harusi)









1. Kujitambulisha ukweni. Hapo utatakiwa uende kijijini alikozaliwa mkeo mtarajiwa ukajitambulishe huko. Kama mfano mkeo anatokea Mwanza, na mnaishi Dar, andaa nauli ya watu wawili, malazi kwa siku mbili, na utagharamia shuhuli hiyo ya utambulisho. We tenga 500,000. Hapo tuna assume mkeo atajitegemea. Otherwise 800,000 itakutoka.

2. Kumtambulisha mkeo kwenu. Kama nyie nyumbani ni Arusha, utatakiwa umpeleke huko Ngarenanyuki. Sio umlete hapo Tabata mlipopanga. Hapo sio kwenu! Andaa nauli yako na atakaekusindikiza, nauli ya binti na mwenzie, na gharama za vinywaji na chakula siku hiyo. Utahitaji kama 700,000

3. Kifuatacho ITV ni kuwaalika wakwe zako nyumbani. Uwatoe watu kama nane Mwanza, uwalete Arusha. Wale, walale, wajisaidie, kwa gharama zako. We acha ubishi, tenga 800,000 tu.

4. Kwani we wazazi wako wanajua unakooa? Sasa je? Wasafirishe kwenda Mwanza! Watu watano. Utahitaji kuwa na 500,000. Beba pia ATM card yako, kuna imejensi.

5. MAHARI ndio topic inayofuata sasa. Ukiwa mjanja, unganishia kwenye hiyo safari hapo juu uue ndege wawili. Pamoja na hayo, itabidi ubebe 2,000,000.

6. Sasa kijana unaweza kumvisha mchumba wako pete. Nunua ya kawaida kabisa ya dhahabu. 350,000. Tukio lenyewe la kumvisha pete unaweza ita marafiki wawili watatu ukatumia 200,000. Au fanya sherehe kabisa. Mi simo

7. Oke, sasa unaweza kuitisha vikao vya harusi. Tengeneza kadi za mwaliko wa kamati kwa 200,000, kikao cha kwanza gharama zote ni juu yako. Andaa 500,000. Swali la kwanza kwenye kikao: “We una shing ngapi?” Sema 1,000,000.

8. Utahitaji 100,000 ya sms na simu kukumbushia michango. (Shukuru Mungu kuna cheka time)

9. Wakati vikao vinaendelea, utatuma 200,000 kwa m-pesa ili mambo ya kimila yaendelee kule nyumbani. We unaelewa

10. “Darling, sasa mi kwenye kitchen party ntavaa nini?” 300,000!

11. “Darling, kuna mahali nimeona gauni zuri la send…” 400,000!

12. “Baby, rafiki yangu alinunua gauni la harusi China yani lilimpende…..” 700,000!

13. Wakati huo wewe mwenyewe hujajua utavaa nini, hujanunua pete za harusi, hujamvalisha best man na mkewe. Tuseme unahitaji kama 1,500,000 maana utalia lia sana. Kumbuka, gharama hizi huchangiwi na kamati. Wala hutarudishiwa.

14. Siku ya send off lazma uende Mwanza. Utaenda mwenyewe? Ndugu wawili watatu na mshenga 600,000. Kwenye send off utatakiwa kutoa sijui blanketi la bibi, vitenge vya mashangazi, na vikorokoro kibao. Nunua hivyo vitu 300,000 uende navyo ili kupunguza gharama. Beba 200,000 za wale mashangazi watakaoibuka ghafla!

15. Mshonee baba mkwe suti 100,000 mama mkwe yeye atavaa gauni la 50,000.

16. Fotokopi hiyo hapo juu (namba 15) kwa wazazi wako. 150,000

17. Watu watakaopenda kuvaa sare wajitegemee! Mimi sina hela! Ila utavishonea nguo vile vitoto kwa 80,000.

18. Siku mbili kabla ya harusi, utaanza kupokea wageni. Unatakiwa uwatafutie malazi na chakula. Kwa ujumla utahitaji kama 500,000

19. Jioni watoe auti mashemeji zako ambao hawajawahi kufika Dar ukawanunulie bia ili wakuone wa maana. 200,000

20. Siku ya harusi bibi harusi na mwenzie na watoto na ma maids watatakiwa wakapambwe saluni. 200,000

21. We na mwenzio mtaenda kunyoa hapo kwa nanii. Ndevu na nywele 10,000

22. Siku ya harusi beba sadaka 10,000. Wakati huo umeshamtuma kijana akakulipie hoteli mtakayofikia baada ya harusi. Kamati haitoi hela hiyo, so utalipa malazi ya siku mbili200,000

23. Kama mtaenda honeymoon sehemu yoyote nzuri nzuri nje ya mji, si chini ya 800,000 kwa angalau siku 5.

24. Wakati uko huko honeymoon, huna hata kumi, mwanakamati mmoja ambae hakuchanga anakupigia simu “ Sasa tunavunja lini kamati?” Pesa yote iliyochangwa ilitumika kwenye harusi, sasa gharama za kuvunja kamati ni za nani?? 500,000!

25. SASA MNAANZA MAISHA YA UNYUMBA. TSHS. 14,150,000/=    poorer. Na hapo makadirio yote nime
weka ya chini.

No comments:

Post a Comment