Thursday, 13 March 2014

WAFAHAMU WAKUU WA WILAYA WALIOACHA HISTORIA , MMOJA ACHAPA WALIMU VIBOKO, MWINGINE AWAPIGIA WANANCHI MAGOTI




Kama uliwahi kusikia mkuu wa  wilaya ya Bukoba, Bwana Albert Mnali aliyewachapa walimu viboko ni huyo mwenye miwani na koti jeusi (aliyezungushiwa duara jeusi) aliweka historia Tanzania,kipindi hicho alikuwa mkuu wa wilaya ya Bukoba na
 taarifa ni kwamba aliwachapa viboko walimu wa shule tatu za Katerero, Kanazi na Kasenene katika mkoa wa Kagera.
 
Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, mkoani Manyara, Anatory Choya akiwa amewapigia wananchi magoti kwa maana ya kuonyesha unyenyekevu
Mbulu. Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, mkoani Manyara, Anatory Choya, amesema kuwa aliwapigia magoti wananchi wa Kijiji cha Hydom, ili kuonyesha unyenyekevu kwa wananchi hao aliodai walionekana kujazwa maneno ya uchochezi na wanasiasa ili wavuruge amani .

No comments:

Post a Comment