KIMEWAKA!
Habari zilizothibitishwa zinaeleza kuwa, sura mbili za mauzo kwenye
sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu na Aunt Ezekiel Grayson wanadaiwa
kula kichapo kutoka kwa msanii mwenzao, Adam Kuambiana, Amani
limeinyaka.
Tukio
hilo lililoshuhudiwa na ‘shushushu’ wetu lilijiri mchana kweupe maeneo
ya Mikocheni, Dar, hivi karibuni baada ya kuibuka timbwili lenye ujazo
wa kilo kadhaa baina ya mastaa hao.
ALIANZA WEMA
Kwa
mujibu wa chanzo, Wema ndiye aliyeanza kummwagia Kuambiana maneno ya
shombo akimwambia kuwa ahakikishe siku hiyo haipiti bila kukata kucha za
miguuni kwani ni ndefu na zinatisha.
“Mwanzoni
ilikuwa kama utani tu. Wema alimwambia Kuambiana akate kucha, tena
itabidi atumie mkasi wa kukatia michongoma maana kwa wembe hazikatiki.
“Pia Wema alimwambia yeye hawezi kumwacha mpenzi wake na kucha ndefu kama hizo za Kuambiana,” kilisema chanzo chetu.
Ilizidi
kudaiwa kwamba wakati Wema akiendelea ‘kumpaka’ Kuambiana, Aunt
aliyekuwa amejilaza chini alidakia na kusikika akisema kuwa ni kweli
msanii huyo mwenye uwezo wa juu katika fani anatakiwa kukata kucha hizo
huku akizungumza maneno ya shombo kwa jamaa huyo.
HASIRA
“Baada
ya kuona imekuwa ‘too much’, Kuambiana alipandwa na hasira, akanyanyuka
kwenye kochi na kumfuata Wema kwa lengo la kumpa kipigo,” kilisema
chanzo hicho.
MARTIN KADINDA AMUOKOA
Habari
zilidai kwamba, Kuambiana alipomfikia Wema alianza kumpiga vibao hadi
meneja wake, Martin Kadinda akaingilia kati kumuokoa mwanadada huyo
ambaye pia ni meneja wake.
KIBAO CHAMGEUKIA AUNT
Chanzo
kilieleza kwamba baada ya kuachana na Wema, msaanii huyo ambaye pia ni
‘dairekta’ wa sinema mbalimbali za Bongo alimfuata Aunt na kuanza
kumlamba makofi ya kutosha.
Tukio
hilo lilizua tafrani na kuwafanya wasanii wengine waliokuwa eneo hilo
wakimbie na kushindwa kuwatetea Aunt na Wema kwa kuogopa kugeuziwa
kibao.
KUAMBIANA ANASEMAJE?
Baada
ya kuinyaka ishu hiyo, mapaparazi wetu walimtafuta Kuambiana na
kumuuliza kulikoni kugeuka bondia na kuwapiga warembo hao ambapo alikiri
kutokea kwa ishu huyo.
Alisema kuwa, Wema na Aunt ni kama wadogo zake, tena yeye kama dairekta wao walipaswa kumheshimu na siyo kumvunjia heshima.
“Akina
Wema ni wadogo zangu, wanahitaji kuniheshimu na mimi ndiye mwongozaji
wa filamu yao, kwa nini wanikosee heshima? Hata kama wamekasirika lakini
nimewashikisha adabu,” alisema Kuambiana kwa ile sauti yake nzito.
WEMA & AUNT
Kwa
upande wao, walipoulizwa Aunt na Wema kuhusiana na kichapo walichopewa
walisema walishamzoea jamaa huyo, lakini kwa alilolifanya la kuwapiga
makofi aliwakwaza kwa sababu hata kama ni mwongozaji wa filamu yao
lakini alikuwa pale kwa ajili yao.
HISTORIA YA KUAMBIANA
Ukiachana
na tuki hilo, Kuambiana anadaiwa kuwa na mkono mwepesi hasa anapokuwa
‘lokesheni’ ambapo mwaka jana, aliwahi kumtia mikononi staa mwingine wa
filamu za Bongo, Rose Ndauka walipokuwa wakirekodi filamu visiwani
Zanzibar.
Siku
ya tukio hilo, Kuambiana alikuwa akidairekti Filamu ya Distress in
Zanzibar. Alimshutumu Rose kuvaa mavazi tofauti na maagizo yake, katika
kujibishana akamuwasha makofi.
HATA MITAANI!
Juni,
mwaka jana, Kuambiana alimshushia kipigo Fadhili Joseph ambaye alimdai
fedha za bia alizokunywa kwenye baa yake, Sinza, Dar es Salaam.
Kuambiana
aliposhindwa kulipa aliacha laptop (kompyuta mpakato), siku iliyofuata
alirudi na kushusha kichapo huku akiitaka laptop hiyo.
Kuambiana
alikamatwa na Polisi Kawe, Dar kwa faili la malalamiko KW/RB/5761/2012
SHAMBULIO. Kesi hiyo ikahamishiwa Kituo cha Polisi Kijitonyama
‘Mabatini’ kwa vile ndiyo kituo cha karibu na eneo la tukio.
MADAIREKTA WAKOJE?
Mbali
na Kuambiana, staa mwingine ambaye pia ni dairekta wa muvi za Bongo,
Issa Musa ‘Cloud’ naye aliwahi kutoa kipigo cha bakora kwa msanii
Blandina Chagula ‘Johari’ kwa kosa la kuchelewa kufika sehemu ya
kurekodia filamu.
No comments:
Post a Comment