Tuzo ya mwalimu bora zaidi duniani imezinduliwa.
Tuzo hiyo yenye thamani ya dola milioni moja,
itakabidhiwa mwalimu ambaye anafanya kazi ya ualimu na ambaye
atathibitisha kuwa mchango wake kwa jamii umekuwa bora zaidi kuliko
walimu wengine wote duniani.
Tuzo hiyo ambayo imezinduliwa na wakfu wa Varkey
Gems, shirika ambalo hutoa mchango mkubwa katika sekta ya elimu
duniani, inaungwa mkono na mtawala wa Dubai, Sheikh Mohammed bin Rashid
al Maktoum.
Mwenyekiti wa wakfu huo ni Rais wa zamani wa
Marekani Bill Clinton. Bwana Clinton amesema kuwa ni muhimu sana
kuwavutia watu bora zaidi kuwa walimu na pia kuwaza kuwathamini na
kuthamini kazi zaO.
Unadhani mwalimu wako anaweza kushinda tuzo hii?
No comments:
Post a Comment