NI
wiki nyingine tulivu kabisa tunakutana tena kupitia ukurasa huu namba
moja kwa kuandika makala kali zinazogusa maisha yetu ya kimapenzi. Ni
matumaini yangu umzima bukheri wa afya na unaendelea vyema na majukumu
yako ya kila siku kama kawaida.
Mpenzi
msomaji wangu, kama ulikuwa hujui ni kwamba mapenzi ya sasa
yameingiliwa! Kama ni muziki basi waswahili wanasema disko limeingiliwa
na Mmasai. Nasema hivyo kutokana na yale ninayoyaona kwenye uwanja wa
mapenzi.
Yaani sasa hivi ni kweli hapendwi mtu bali pochi lake lililonona. Kuna walioingia kwenye uhusiano na watu ambao kiukweli hawana mapenzi nao ila pesa imewasukuma.
Wapo waliokubali kuingia kwenye ndoa na watu ambao katika mazingira ya kawaida wasingekubali lakini kwa sababu ya mali na pesa wameshawishika.
Hata hivyo, si wote walioingia kwenye penzi kwa kufuata pesa wana furaha maishani mwao. Wengi wao sasa wanajuta, wanahisi wamefanya makosa makubwa kuyaacha maisha yao ya kimapenzi yashikiliwe na pesa.
Ukweli ni kwamba, pesa na mapenzi ni vitu viwili tofauti ambavyo hata kama vina uhusiano wa karibu lakini mapenzi yanaweza kuwepo hata kama pesa haipo.
Wanaofuatilia historia wanajua kuwa, enzi hizo mababu na mabibi zetu hawakuwa wakijua pesa lakini mapenzi waliyokuwa wakioneshana yalikuwa ya aina yake. Walipendana kwa maana halisi ya kupendana kutoka kwenye mioyo yao.
Sasa hivi mambo yamegeuka, pesa imekuwa ikitangulizwa mbele kwenye suala la uhusiano na matokeo yake sasa mapenzi yanakuwa ya kimaigizo. Mtu hakupendi lakini anaonesha kukuzimikia ile mbaya kwa sababu tu ameona pochi limetuna, likisinyaa na yeye anaingia mitini.
Mbaya zaidi sasa hivi wapo ambao wamekubali wadhalilishwe na wafanyiwe kila aina ya unyanyasaji eti tu kwa kuwa wamedondokea kwa mtu mwenye nazo. Hiki ndicho nilichopanga kukizungumzia leo.

Hivi karibuni niliongea na dada mmoja ambaye alinisimulia kisa cha kushangaza sana kuhusu mpenzi wake. Kwa maelezo yake ni kwamba, mpenzi wake ana pesa nyingi lakini cha ajabu amekuwa akimdhalilisha katika maeneo mbalimbali, hebu msikie;
“Familia yetu ni maskini na baada ya kumpata yule kaka, alikuwa akiihudumia familia yangu kwa ujumla. Nilikuwa nikimpenda na hata alipoonesha ubinadamu wake wa kuijali familia yangu nikaongeza mapenzi.
“Kinachoniumiza mimi ni kwamba, kila ninapokutana naye ananilazimisha nimpe mapenzi kinyume na maumbile. Ninapomkatalia, ananikasirikia na inaweza kupita hata wiki bila kuwasiliana.
“Mbaya zaidi huwaambia ndugu zangu kuwa namkorofisha na wao hunijia juu. Kusema ukweli huyu kaka
ananidhalilisha na ukimuangalia huwezi kuamini kama anaweza kuniomba kitu kama hicho.”
Maelezo ya huyu dada yalinipa simanzi, nikagundua kwamba kwa hali ngumu ya maisha iliyopo wapo ambao wanakubali kudhalilishwa na wapenzi wao kwa sababu ya pesa.
Huko mtaani wapo wanaokubali kufanya mapenzi kinyume na maumbile eti ili wasije wakaachwa, huu ni ulimbukeni!
Hata kama ana pesa zake lakini asizitumie kukufanya wewe chochote anachokitaka.
Kwa kifupi kulazimisha mapenzi kinyume na maumbile ni kujidhalilisha sasa kama unaye mpenzi ambaye anakulazimisha kufanya mchezo huo na kwa kuwa na wewe una shida zako unakubali, unakosea sana.
Jitathmini na usijirahisi kwa sababu ya pesa.
Wanawake wasiwape wanaume nafasi ya kuwadhalilisha kwa sababu ya pesa zao. Wanaume nao wawe na utu, watambue kufanya mapenzi kinyume na maumbile kuna madhara makubwa kwao na kwa wanawake pia.
Ni hayo tu kwa leo.
No comments:
Post a Comment