Uchunguzi
wa utafiti kutoka chuo kikuu cha Exeter nchini Uingereza, unapendekeza
kuwa idadi ya mbegu za uzazi za wanaume huathiriwa kwa kuweka simu za
mkononi kwenye mifuko ya suruale
Hata hivyo
,mwana sayansi wa maswala ya uzazi na shahawa,alisema kuwa ushahidi huo
bado haukuwa na uhakika wowote hivyo basi simu yake bado inaendelea
kukaa mfukoni mwake.
Lilichanganua
tafiti kumi tofauti kuonyesha ubora wa shahawa ikihusisha wanaume
1,492.Hii ilijumuisha kupimwa kwa shahawa zilizowekwa wazi kwa
mnunurisho wa simu za rununu, kwa maabara na udadisi wa wanaume katika
cliniki za uzaziUchunguzi huo uliochapishwa katika jarida la
'Environment International' ulilaumu mnunurisho wa kielectromagnetiki
kuwa chanzo kikuu.
Kiongozi wa
uchunguzi huo Dkt.Fiona Mathews aliambia BBC kuwa kutokana na uchunguzi
huo,moja tu ndio ulionyesha uhusiano kati ya utumizi wa simu na
kudidimia kwa ubora wa shahawa.
"Nafikiri
kwa mwanamume wa makamu hakuna haja ya kuingiwa na hofu,iwapo unajua una
uwezekano wa kuwa na shida ya kizazi basi itakuwa jambo la busara
kutoweka simu mfukoni ,pia kugeuza mtindo wako wa kula."
Mbegu za uzazi za wanaume zinasemekana kuathirika kutokana na simu za mkononi
'Uchunguzi zaidi'
Alikubali kukosolewa na wana sayansi wengine huku akiunga mkono kuwa kuna umuhimu wa kufanya uchunguzi zaidi.
Dkt,Mathews
alimaliza kwa kusema"hili ni jambo la kusisimua lakini hatusemi kwa
uhakika kuwa kila anayebeba simu mfukoni atakuwa na shida ya kizazi.
"
Dkt.Allan
Pacey kutoka chuo kikuu cha Sheffield anasema kuwa wazo hilo la
kudidimia kwa shahawa na kuharibu "DNA"linatokana na "radio frequency"
na mnunurisho wa kielectromagnetiki zinazopatikana kwenye simu na
pengine joto aidha moja kwa moja kutoka kwenye simu au mnunurisho.
Dkt huyo
anayefanya uchunguzi wa shahawa bado hajashawishika akisema ushahidi huo
hauna msingi na ataendelea kuweka simu mfukoni.
Aliambia
BBC,"kumekuwa na shauku kwa mda kama kuweka rununu mfukoni kunaweza
changia kudidimia kwa ubora wa shahawa na nguvu za kiume kivyovyote.
"Kumekuwa na
habari zisizokuwa na msingi lakini kwa maoni yangu uchunguzi uliofanywa
hadi kufika sasa haujakuwa wa kutosha kwa sababu wachunguzi aidha
hawakuhifadhi shahawa vile inavyofaa ama wamedadisi matumizi ya simu
kati ya wanaume bila kuzingatia mambo mengine kama mitindo yao ya
maisha.
"Tunayohitaji ni uchunguzi kufanywa ambapo utumizi wa simu unazingatiwa vile vile tabia zinazoathiri maisha yao.
Hadi pale tutakapo tafakari hayo,nitaendelea kuweka simu yangu katika mfuko wa mkono wa kulia wa suruale yangu!"
No comments:
Post a Comment