Wednesday, 29 January 2014

HII NDIYO MAANA YA MSTARI WA "ZITTO AKILOGA KASULU SISI TUNAMLOGEA PANGANI" SOMA ALICHOFUNGUKA ROMA HAPA



 
Mara nyingi mistari mingi katika nyimbo za HipHop humfanya msikilizaji atumie akili nyingi sana ili kuelewa msanii alimaanisha nini katika wimbo huo. Mfano mzuri wa wasanii ambao ukisikiliza nyimbo zao kuna baadhi ya mistari lazma ufikiri sana hadi uje uielewe ni Roma Mkatoliki. Mfano wa mstari ambao uliwatoa jasho wengi ni "ZITTO AKILOGA KASULU SISI TUNAMLOGEA PANGANI"
 
Kupitia website yake Roma Mkatoliki ameelezea maana ya mstari huo kwani wengi walikua wakiutafsiri kwa maana tofauti kabisa. Na hiki ndo alichokisema Roma.
 
BANDARI CHANUU!! RAILWAY CHALII!! MAKAMBA IINUE KATANI/ ZITTO AKILOGA KASULU SISI TUNAMLOGEA PANGANI/ 
 
 Meanz- Miaka ya nyuma jiji letu la tanga lilikuwa ni miongoni mwa sehemu/mkoa ambao tanzania inajivunia kwa kujipatia pato kubwa kutokana na kilimo cha zao la katani!! 
 Ulikuwa ni mkoa ambao upo katika maendeleo na utajiri mkubwa kutokana na
 BANDARI NA RILWAY!! 
 Wagosi waliimbaga " 
RELWE KIMYAAA, 
 ZAMANI WENYEWE PALE TUSHAZOEA MIJIHONIII,
 SASA HIVI? BEHEWA MOJA LA ABIRIA HATULIONI, 
 MWAEKANI BASI MABEHEWA YALOOZANA PALE? 
 SI WAONDOE JAMA YAWEKA MAFICHO YA WEZI YALEEE EE 
TANGAA KUNANI PALEEE!!!?
 
 Hao ni wagosi wa kaya kaka mkoloni na dr john,
 waliimba hivo miaka ya nyuma, na hadi leo bado hivi vitu havipo ktk hadhi ya miaka ileee,  
 
ndomana nikasema bandari imeanguka CHANUU!!
 relwe imelala CHALII!! nikimaanisha vyote vimekufa na sio kama zamani!!
 
 hali hii imepelekea tanga imedoda(imeshuka kimaendeleo)!! 
 KATANI nayo ikaja ikashuka sana na sio kama zamani, 
 zao hili ndo lilitegemewa sana mkoani hapa kwetu tanga!!! 
 Sasa basi mh JANUARI MAKAMBA ndugu yetu kipenzi wa tanga, hongera kwa kasi yake ya kazi, aliyonayo , ni mfano wa kuigwa!! huwa akiliongelea sana hili la kuiinua TANGA,
 
 na hata kutia nguvu kwenye kilimo cha katani, kuiinua bandari na relwe pia na nyanja zingine!!
 
 So kupitia muziki wetu/wangu(HIP HOP)nafahamu sana kuwa muheshimiwa huyu ni mpenzi sana wa muziki, 
 
so nilijua kupitia muziki itamuhamasisha yeye na wananchi wa tanga na watu wengine wote kulitilia mkazo na kuwekeza nguvu zao ktk hili ili TANGA irudi kwenye kilele cha maendeleo bora!! Ndio maana ya MAKAMBA na watu wake waliomzunguka,(angeweza kuwepo yoyote anayehusika na huku, awe mbunge, 
meya hata mkuu wa mkoa!!maana maendeleo sio hayo yaliyotajwa tu!!)WAIINUE KATANI, RELWE, BANDARI na vyote vilivyotuzunguka ambavyo ni kama rasilimali kwa jiji letu TANGA!! Zitto akiloga kasulu sisi tunamlogea pangani!!
 zitto mh. mbunge wa kgm kaskaz!!! 
 ni mpiganaji/mchapa kazi/kiongozi mwenye uchu wa maendeleo ya taifa!!
 
 anafanya mengi kuyadhihirishaga haya!!
 Kasulu na pangani ni kama figure zinazowakilisha kigoma na tanga respectively!!!
 
 na mh zito naye ni miongoni mwa viongozi wanaopenda na kusapoti sana muziki wa kizazi kipya(na ndio muziki ninaoufanya mimi)tumeona lekadutigite ni movement nzuri na wengi tunatamani iigwe na viongozi wengine!! na hata kwa mh zitto tunaomba isiishie kigoma tu akiweza aiendeleze kwa wasanii wengine wa sehemu tofauti!! So nilijua kupitia muziki (HIP HOP) ambapo naye ni mpenzi wa muziki, 
 
basi itakuwa rahisi kulifikisha hili kwake na kwa wote!! amefanya maendeleo kigoma wameona na bado anaendelea kuwafanyia hayo!! Sasa neno kuloga limetumika kwasababu tumehusisha tanga na kigoma hapo!! na mnajua ni mikoa yenye umaarufu kwa mambo hayo toka enzi!!
 
 "lazima lingeleta usikivu na watu kuisogelea sauti hii" 
 Lakini TAFSIRI YA NENO HILO HAPO KULOGA NI = MAENDELEO!!
 
 MH ZITO AKIFANYA MAENDELEO KIGOMA NASISI KINA MAKAMBA TUKAMUONYESHE KUWA HATA SISI TWAWEZA KUWEKA LAMI SAFI HADI PANGANI!!
 NA MAENDELEO MENGINE KAMA HAYO!!!
LIMETUMIKA NENO KULOGA LIKIWA NI USANII WA KULETA UHUSIANO WA MIKOA HII INASIFIKA KWA HAYO MAMBO!!
 
 LAKINI Pia neno kuloga hutumika kama kitu kizuri sasa hivi na tunaelewana tu masela mfano
 "duh linex ngoma yake imewaloga wote" 
 haina maana kuwa kaloga kwa mganga!! la hasha!!
 ni msemo tu kuwa kafanya kilicho bora zaidi ya wenzie. 
 
 LEO IKISEMWA HIVI- MR NICE ATAWASHA MOTO LEO DAR LIVE!! 
 
 kwahiyo watu waje na zima moto kuwa atauwasha moto au? basi na police wamkamate kafanya kosa la kuwasha moto!! 
 AU ISEMWE - LEO JUMA NECHA KAFANYA SHOW YA KUFA MTU!!
 
 so necha afungwe maana kaua mtu? 
 BASI NI LUGHA TU HZI HUTUMIKA KISANII NA WAELEWA SANA WA MUZIKI WA HIP HOP WATAELEWA MAPEMA NA KWA WEPESI,  
 
WASIO WAELEWA NI MUDA WA KUPATA DARASA KWA ROMA!!
 SO BIG UP MH ZITO KABWE KWA KUISIMAMIA KIGOMA VIZURI MUNGU AKUBARIKI SANA NAFURAHIA UNACHOKIFANYA!! 
 BIG UP MH JAN.
 MAKAMBA KATIKA HARAKATI ZA KUISIMAMIA TANGA YETU MUNGU AKUSIMAMIE NAWEWE UTIMIZE NDOTO HIZI NJEMA!!
 LENGO NI KUWA IKIFIKA 2030 TANGA NA KIGOMA NA KOTE TANZANIA TUWE TUPO MBALI KIMAENDELEO.....
NA TUJE TUJIVUNIE KUWA HIP HOP ILISAIDIA KULETA UKOMBOZI WA MTOTO, 
KIJANA HADI MZEE TANZANIA YETU. HIP HOP(MOVEMENT) Roooomaaaaaa!!!!

No comments:

Post a Comment