Thursday, 16 May 2013

JE UNAJUA JINSI YA KUTENGENEZA JUISI YA UBUYU???soma hapa.........

003

Miaka hii yakaribuni ubuyu umekua tunda lenye jina kubwa sana kwenye jamii yetu ya kitanzania,unasifika kwa kua na virutubisho vingi hasa calcium na Iron
Ubuyu hufaa sana kwa Wajawazito,watoto na wazee,kwani makundi haya yanauhitaji mkubwa wa calcium na iron.
Namna nzuri na rahisi ya kufanya ubuyu sehem ya lishe  ni kwa kuutumia kutengeneza juisi
Juisi ya ubuyu imekua maarufu sana katika jamii yetu na inapendwa sana.Mimi mwenyewe ni mmoja wa wapenzi wakubwa wa juice ya ubuyu.Ingawa unaweza changanya ubuyu na matunda mengine,mimi napenda kunywa juice ya ubuyu pekeyake.Wakati mwingine naiwekea rangi na kuongezea vanila ili tu kuipa sura na harufu ya tofauti.
Watu wengi hawachemshi juisi ya ubuyu,Jambo ambalo ni hatarishi ki afya.Chemsha ubuyu ili kuuwa vijidudu viletavyo magonjwa,ubuyu hupita kwenye mikono ya wengi kabla haujakufikia wewe mtumiaji,na pia hujui ulitunzwa katika mazingira gani.Ni vyema kuchukua taadhari kwa kuchemsha.
Mahitaji
Ubuyu(wa unga au wa mbegu)
Maji
Sukari
Njia
1.Chambua ubuyu,ondo uchafu wowote uliopo kwenye ubuyu
2.Katika sufuria,weka ubuyu kisha ongeza maji.Katika kila kipimo cha ubuyu ongeza maji mara tatu yake
  • Ubuyu wa mbegu vikombe 6  weka maji vikombe 9
  • Ubuyu wa unga  vikombe 3 weka maji vikombe 12
3.Funika sufuria kisha bandika jikoni,chemsha adi vitokote,vipe  angalau dakika nne za kutokotea.
002 
  • Kumbuka maji unayotumia kuchemsha ubuyu ni maji ya bomba na si salama,hivyo ni muhim kuyapa  muda mzuri wa kuchemka ili juice yako iwe salama.
4.Juisiinapoanza tu kutokota ongeza sukari kwa ladha uipendayo kisha acha zile dakika nne za kutokota ziishe.Zima jiko acha juisi ipoe.
  • Napenda kuweka sukari ichemkie kwenye juice kwani inafanya juice ishikane na kua nzito.Sukari ikichemshwa inakawaida ya kua nzito.Kumbuka kwamba ubuyu ni mwepesi sana na juice yake kawaida hujitenga inapotulia,ubuyu waenda chini na maji yanabaki juu.Ukichemsha sukari inasaidia kuondoa hali hiyo.
5.Chuja juisi,ongeza maji kama unaona ni nzito sana,na ongeza sukari endapo ile uliyoweka awali haitoshi.Juisi tayari kwa kunywa.
006 
Maelezo ya ziada.
Kama unampa mtoto mdogo juice hii,basi acha itulie ili unga au chembechembe za ubuyu ziende chini,kisha chukua juisi nyepesi iliyobaki juu nsio umpe mtoto.Juice ya ubuyu nzuri sana kwa mtoto kwani ina calcium kwa wingi.



No comments:

Post a Comment