Thursday 16 May 2013

MWANAMKE JIKO-Wanawake,kinadada na mabinti wa leo mnatia aibu.


Chakula ni sehem kubwa sana ya maisha yetu ya kila siku ,na jamii imeliweka  jukumu la kuandaa chakula  mikononi mwa mwanamke.Tangu enzi za mababu zetu swala zima la uandaaji wa chakula limekua mikononi mwa Mwanamke.Kwa maana hiyo basi kuna ulazima mkubwa sana wa mwanamke kujua kupika au kuandaa chakula.Ni wazi kwamba moja kati ya sifa za mwanamke mzuri ni kujua kupika,uzuri wa sura pekee hautoshi.Waswahili wana msemo usemao AMEPATA JIKO unaomaanisha kwamba ameowa au amepata mke,msemo huu umeweka wazi kabisa kwamba mwanamke na jiko ni wamoja,alipo mwanamke basi jiko nalo lipo.Jiko ni fahari ya mwanamke,ndio eneo lake la kujidai,hapo ndipo pakuonyeshea manjonjo yako.
Miaka hii ya karibuni wanawake na mabinti wameingia dosari kubwa ya kutojua kupika,mabinti wengi wa miaka hii hawajui kupika na wengi hata hawaoni kama hilo ni tatizo kwa upande wao.Wanawake wamesahau nafasi yao na majukumu yao jikoni.Kumekua na kasumba ya kuacha dada wa kazi apike chakula cha familia kila siku,jambo ambalo si sawa kabisa.Ukiwa kama mama katika familia ni lazima ujipange ili upate muda wa kuipikia familia yako,Hata kama uko bize sana na kazi siku za wiki basi wikendi jitose jikoni au zile siku unazobaatika kufika nyumbani mapema  ingia jikoni,Dada wa kazi anaweza kukuandalia kila kitu na unapofika unafanya kuupika tu.

 
Utakubaliana na mimi nikisema Kutojua kupika au upishi mbaya wa wanawake  umekua chanzo cha malumbano,kutoelewana na kuporomoka kwa mapenzi katika ndoa nyingi.Pale ambapo mama hapiki kabisa au basi anapika vibaya ndio mwanzo wa baba kupita kula mtaani kabla ya kwenda nyumbani,na katika safari hizo za kula mtaani kina Hadija na Neema nao wanamsogelea na  ikitokea baba akakutana na mwanamke mwingine anaejua kupika,atakaribishwa mlo leo na kesho na mwisho atahamia uko kabisa.mambo ya aibu haya jamani.Kwa upande mwingine,watoto nao hali zinakua mbaya,afya zinakua dhaifu kwasababu mama hapiki  au hapiki vizuri Nyumbani.
 
Ninapoongelea kupika chakula kizuri  haimanishi kwamba upike chakula Fulani cha ajabu,inamaanisha kile chakula unachopika cha kawaida kabisa basi kipike kwa umakini na kukipa vionjo vinavyoleta ladha nzuri inayovutia.Nitoe mfano wa wali na maharage.unaweza kupika wali na maharage wiki nzima na kila siku ukapika kwa style ya tofauti kitu ambacho kinafanya walaji wasichoke kula chakula kile kile kwani kila walapo wanakutana na ladha ya tofauti na ile waliokula jana.Na pia inampa baba sababu ya kutaka kuwai nyumbani atokapo kazini kwani hajui mama kaandaa nini kizuri jikoni,lakini pale ambapo mtu amekariri  au anajua atakuta kimepikwa nini na kimepikwaje basi ata ile hamu ya kuwai nyumbani kula inaisha.Hata watoto pia huchoka kula chakula kilekile na mapishi yale yale ndio maana baadhi ya watoto hawapendi kula ,si kwamba hawana hamu ya kula,ila wamechoka kula kitu kile kile.
 
Ivi unajua kua wanaume na watoto wanapokua katikati ya rafiki zao hupenda kujivunia upishi wa wake zao/mama zao?hujawai ona mototo anaficha chakula ili ampelekee rafiki yake?au anaomba afungashiwe chakula ili apelekee rafiki zake?umewai kutana na mwanaume anaependa kukaribisha watu kwa ajili ya chakula nyumbani kwake?au mwanaume ambae anawai nyumbani ili akale na familia?ushawai kutana na mwanaume ambae mara nyingi hukosoa chakula anapokula nje ya nyumbani kwake?hizi zote ni dalili zinazoonyesha mama au mke ni mpishi mzuri.
Baba yangu aliwai kutuchekesha kwamba,aliwai kukaribishwa kwa ajili ya chakula cha jioni nyumbani kwa rafiki yake enzi zileee,mama wa familia hiyo alijikunja kweli kumpikia mgeni lakini alipokaribishwa meazani ,hakuweza kujizuia kuushangaa mchuzi.nanukuhu maneno yake ”nyanya huku kitunguu kule vinaelea juu yamchuzi,mchuzi mweupe adi unaona yale maandishi ya made in china yalioandikw ndani ya bakuli ”.
Jamani kina mama,dada na mabinti ni aibu sana kwa mwanamke kutokujua kupika,kupika ni fahari ya mwanamke na inakupa jina la kuringia.kua mzuri,mrembo mwenye adabu tele,msomi na hela za kumwaga alafu jikoni sifuri ni aibu tupu.Jifunze kupika,kua huru kuuliza au kuomba kufundishwa kupika na ndugu,jamaaa na marafiki.Si aibu kutokujua ni aibu kutotaka kujua.Unaweza dharau haya ninayoyasema lakini mwisho wa siku wakati ndoa yako inasuasua na wanao afya zinatia aibu utanikumbuka.kabla hujafikia atua hizo tafadhali chukua Atua.



No comments:

Post a Comment