Wednesday, 22 May 2013

Ripoti ya Vodacom kumtia Lema kitanzani tena........


bunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya (Chadema) Godbless Lema akiwaa chini ulinzi wa Polisi.


Arusha,Tanzania
SIKU moja baada ya Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom kusema kwamba, ujumbe mfupi wa simu ya mkononi ambayo Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema) Godbless Lema alidai kuwa ametumiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo si ya kweli,Mbunge huyo huwenda akaongezea mashtaka.
Katika ujumbe huo Mbunge huyo alidai kwamba Mulongo alimtumia ujumbe mufupi uliosomeka kwamba, "Umeruka kihunzi cha kwanza,nitakuonyesha mimi ni Serikali, ulikojificha nitakupata na kukupa kesi ninayotaka mimi, "ilisema sehemu ya ujumbe huo.
Wakati Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Liberatus Sabas akitangaza kwamba ujumbe huo haukutumwa na mtumiaji wa simu za makampuni ya simu Tanzania, bali ilitumwa na makampuni za nje ya nchi, duru za ndani ya jeshi la Polisi zinadai kwamba, huenda Mbunge huyo akabadilishiwa mashtaka ama kuongezewa mashtaka mengine, kutokana na taarifa zilizotangazwa na jeshi hilo kutoka Vodacom kwamba ujumbe wa maandishi ya vitisho aliyotumiwa Mbunge huyo na mtu aliyedai kwamba ni Mkuu wa Mkoa huo si za kweli na kuongeza kasi katika shtaka la uchochozi.
Kamanda Sabas alisema, "Uchunguzi wa awali wa Jeshi la Polisi kufuatia tuhuma hizo ambazo Mkuu wa Mkoa Mulongo kukanusha ujumbe huo uliodaiwa kutumwa kupitia namba ya simu ya Mulongo kwenda kwa Lema". Katika kesi inayomkabili Mbunge huyo itakayosikilizwa tena Mei 29 mwaka ni pamoja na shitaka la kuwaambia wanafunzi wa chuo cha uhasibu alipokwenda kuwatuliza kuwa ‘dhambi kubwa kuliko zote ni woga ‘.Haki hutafutwa na kupiganiwa ikiwa jambo unalipigania ni la msingi na linafaa kupiganiwa. Kosa la pili ni pale alipotamka kuwa "Tumemtafuta mkuu wa mkoa juu ya Matatizo yenu na mlivyoshuhudia hapa amechukua muda mrefu na kuingia kama vile anaingia kwenye send-off.

No comments:

Post a Comment