Serikali imeendelea kuongeza kodi kwenye magari makuukuu, bia, vinywaji vikali, na baridi kama ambavyo kodi imekuwa ikifanya kila mwaka na kuwaathiri watumiaji.
Kutokana na hali hiyo wanywaji
pombe na sigara pamoja na waagizaji magari watalazimika kutumia fedha
nyingi zaidi ili kupata huduma hizo.
Vilevile baadhi ya
bidhaa zisizokuwa za mafuta nazo zimefanyiwa marekebisho na kuongezwa
kodi, ikiwamo mvinyo, pombe, vinywaji vikali, na sigara.
Vinywaji
hivyo vimeongezwa kodi kwa asilimia 10. Kutokana na bajeti ya mwaka
2013/14 iliyosomwa jana bungeni na Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa,
vinywaji vikali vimepanda kutoka Sh2,392 hadi Sh2,631 kwa lita, sawa na
ongezeko la Sh239 kwa lita moja.
Bia inayotengenezwa kwa
nafaka nchini ambayo haijaoteshwa imeongezwa kodi kutoka Sh310 kwa lita
hadi Sh341, sawa na ongezeko la Sh31 kwa lita.
Pia bia
nyingine zote zimepanda kutoka Sh525 kwa lita hadi Sh578, sawa na
ongezeko la Sh51 kwa lita. Kuhusu ushuru magari, umeongezwa kwenye
magari yasiyozalisha na yenye umri wa miaka 10 kutoka asilimia 20 mpaka
hadi asilimia 25.
Dk Mgimwa alisema hatua hiyo imelenga kupunguza uagizaji wa magari chakavu ili kulinda mazingira na kupunguza ajali za mara kwa mara, huku ikiongeza mapato kwa Sh510 bilion
No comments:
Post a Comment