H Baba na mkewe Flora Mvungi katika pozi.
Wawili hao walifungishwa ndoa na Shehe Maulid katika Msikiti wa Kibo,
uliopo Ubungo, Dar, Jumamosi iliyopita na baada ya ndoa kufungwa
sherehe ilifanyika nyumbani kwa akina Flora maeneo ya Kibo.
Tumefurahi
sana na tunamshukuru Mungu kwa kuwa tumetimiza ndoto yetu kwani maneno
yamesemwa mengi sana juu ya uhusiano wetu lakini Mungu ameendelea
kutuweka pamoja mpaka tumefunga ndoa”.
Flora akimnywesha mumewe kinywaji.
Baada ya watu kula na kunywa na maharusi kusaini vyeti vya ndoa,
waliondoka kuelekea nyumbani kwao Mikocheni, Dar ambako kulikuwa na
sherehe ya maulidi kulikokuwa na vyakula na vinywaji vya kutosha.
H Baba akisaini kitabu cha ndoa.
Akizungumza na mwandishi wetu, H. Baba alifunguka kuwa aliamua
kutokufanya sherehe ukumbini kutokana na wazee wake kukataa kwani kwa
dini ya Kiislamu hairuhusiwi kufanya sherehe ukumbini ndiyo maana
wakaamua kufanya maulidi tu.
Flora naye akisaini kitabu cha ndoa.
No comments:
Post a Comment