MAHAKAMA
ya Wilaya ya Iramba mkoani Singida umemhukumu mwanamke mmoja mkazi wa
kijiji cha Kisana wilayani humo, Sayuni Ramadhani (42) kwenda jela
miaka mitatu baada ya kukiri kosa la kumng’ata mumewe sehemu zake za siri.
Mwendesha
mashitaka mkaguzi wa polisi, Vincent Ndasa alidai mbele ya hakimu
mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Iramba, Kariho Mrisho kuwa Juni 4
mwaka huu saa 12.00 jioni katika kijiji cha Kisana, mshitakiwa kwa makusudi alizing’ata kwa meno sehemu za siri za mume wake, Onesmo Nathania (42) na kumsababishia maumivu.
Ndasa alidai kuwa siku ya tukio, wanandoa
hao waliporejea nyumbani kutoka kwenye klabu cha pombe ya kienyeji
kijijini hao, kulitokea kutokuelewana na hivyo kuanza kugombana.
Alidai
wakati wanaendelea kupigana, Onesmo alizidiwa nguvu na kuangushwa
chini na mkewe ambaye alifungua zipu ya suruali na kufanikiwa kuzitoa
sehemu za siri za mumewe na kuzing'ata nusura azitenganishe.
Mwendesha
mashitaka aliendelea kudai kuwa mlalamikaji Onesmo alipiga yowe na
majirani walifika mara moja na kumkimbiza katika zahanati ya kijiji kwa
ajili ya matibabu.
Mshitakiwa alipoulizwa iwapo ni kweli alikiri
kosa na akaiomba mahakama imwonee huruma kwa kumpa adhabu ndogo kwa
kuwa hilo lilikuwa ni kosa lake la kwanza na kwamba anahitaji kuwa na
mumewe ili waendelee kulea idadi kubwa ya watoto wao kwa pamoja.
Naye
mwendesha mashitaka, Ndasa aliiomba mahakama kumpa adhabu kali
mshitakiwa ili kuwa fundisho kwake na pia kuogofya wanawake wanaotarajia
kuwafanyia unyama wa aina hii ya kung’ata sehemu nyeti za waume zao.
Akisoma
hukumu hiyo, Hakimu Mfawidhi Mrisho, alisema mahakama yake imezingatia
kwa makini maombolezo ya mshitakiwa na kufikia uamuzi wa kutoa adhabu
ya kutumikia jela miaka mitatu.
No comments:
Post a Comment