B12 akiwa amemshika nyoga mtoto mkali ambae hakufahamika jina lake hivi karibuni.
Mirrad Ayo akiwa kwenye moja ya shughuri zake za utangazaji kuripoti matukio, Lakini kwa sasa hali imekuwa tofauti kwa mtangazaji huyo ambae hawezi kujichanganya sehemu yoyote yenye mkusanyiko wa mashabiki bila kuwa na ulinzi wa mabaunsa.Hali inazusha minong'ono mingi kwa mshabiki.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida na
kushangaza watangazaji wa kituo cha radio Cluod Fm cha Jijini Dar wiki
iliyopita waliwaacha watu midomo wazi kwa hatua ya mtindo wa kutembea na
mabaunsa maalum wa kuwalinda wakati hawakuwa na utamaduni huo toka
awali.
Mwandishi wetu aliyekuwa ndani ya
viwanja hivyo alishuhudia watangazaji hao Mirrad Ayo na B 12 wakiwa
chini ya usalama mkali wa mabaunsa hao na kusababisha kuzua
minong'ong'ono kibao kwa mashabiki huku wengine wakihusisha sababu za
kujiwekea ulinzi ni kutokana na mabifu yaliyopo sasa kati ya baadhi ya
wanamuziki na uongozi wa kituo hicho namba moja cha burudani Afrika
Mashariki na kati.
Hata hivyo mmoja wa mashabiki wa muziki wa kizazi kipya mkoani humo aliyejitambulisha kwa jina la Mkude alisema "Matokea haya ya watangazaji kutembea na walinzi wakati hawakuwa na kawaida hiyo awali ni matokeo mabaya sana na inaonesha dhahiri kuwa hata mshabiki hawafurahishi kusikia kituo hicho kikiingia kwenye migogoro na wanamuziki ambao kimsingi wananguvu kubwa sana kwenye jamii kuliko chombo chochote cha media" Alisema kijana huyo.
Aidha nae mdau wa muziki wa kizazi kipya Mkoani Morogoro na Katibu Tarafa Uranga na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa taifa CCM Maliki Marupu ambae aliongea na mwandishi wetu alisema kuwa ni vyema uongozi wa radio hiyo ukakaa chini na kutafarakari kuondoa tofauti zilizopo kati yao na wanamuziki ili kurudisha imani yao kwa mshabiki ambao kwa sasa wameghathirika kutokana na utofauti huo.
No comments:
Post a Comment