Sunday, 30 June 2013

OFISI YA CCM WILAYA YA MBINGA YACHOMWA MOTO



  Katibu wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Mbinga Anastasia Amasi akionyesha sehemu iliyoanzia moto kuwaka na kukamata  pazia.

  Kama unavyoona katika picha hapo ni ndani ya ofisi baada ya moto kuwaka

Katibu wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Mbinga Anastasia Amasi anayeonekana katika picha akitoa  maelezo kwa nje ambapo walimwaga mafuta aina ya petroli dilishani na kuwasha moto
 Huu ni mlango uliomwagiwa mafuta katika upenyo kisha kuwashamoto ambao haukuleta madhara kama ilivyo kusudiwa na wachomaji.



WATU wasiojulikana wamechoma moto jengo la ofisi ya Chama cha Mapinduzi wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma..
 

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo katibu wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Mbinga Anastasia Amasi amesema kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Juni 21 mwaka huu ambapo watu wasiojulikana walichoma moto moja ya jengo la ofisi za chama hicho wilayani humo  .

Moto huo ulielekelezwa katika chumba cha ofisi ya katibu ambapo walivunja vioo na kuchoma moto mapazia lakini kabla hawajachoma vitu vilivyokuwemo ndani walikimbia na kuacha dumu lililokutwa likiwa na mafuta aina ya petroli.
 

Alisema kuwa mpaka sasa hakuna hisia zozote zinazohusiana na tukio hilo ingawa uongozi wa chama cha mapinduzi wilayani humo umeshatoa taarifa kwenye vyombo ya ulinzi na usalama ambavyo vinaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.
 

Katika hatua nyingine , hali ya sintofahamu imejitokeza katika uchaguzi wa viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Mbinga baada ya halmashauri hiyo kugawanywa na kuzaliwa kwa halmashauri mpya ya wilaya Nyasa kwa kuibuka kwa vitendo vya hujuma vinavyodaiwa kufanywa dhidi ya  mgombea mmoja wa nafasi ya mwenyekiti jina lake kuenguliwa katika mazingira ya kutatanisha na kuzua maswali mengi miongoni mwa madiwani wa halmashauri pamoja na wananchi na kutaka uchaguzi huo usifanyike mpaka majina yote matatu ya wagombea yawepo.
 

Mmoja wa wananchi wa halmashauri hiyo ya wilaya ya Mbinga ambaye pia ni katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi  wa kata ya Mbinga mjini Monika John alisema kuwa hizo ni dalili za kuwepo kwa njama za wazi za kupanga safu ya uongozi ambao siyo chaguo la walio wengi bali ni chaguo la baadhi ya viongozi wa halmashauri hiyo kwa masilahi yao.
 

Akizungumzia hali hiyo katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Mbinga alisema kuwa uteuzi wa wagombea wa nafasi hizo hufanywa kwa kuzingatia kanuni za chama na wenye jukumu la mwisho  la uteuzi ni uongozi wa chama ngazi ya mkoa  na yeye si msemaji wa maamuzi ya ngazi mkoa ingawa amepokea tarifa ya kusitishwa kwa uchaguzi huo mpaka taarifa nyingine itakapotolewa na ofisi ya chama ngazi ya mkoa.

No comments:

Post a Comment