Wednesday, 5 March 2014

TUNDU LISSU AMKUBALI SITTA

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA) amesema ameupokea kwa furaha, uteuzi na uamuzi wa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta wa kugombea Uenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba.

Lissu amesema uadilifu na misingi mizuri aliyonayo Sitta itasaidia kupata Katiba ya wananchi badala ya ile ya masilahi ya chama au ya kundi la watu wachache.

Tundu alisema kwa kuzingatia hayo, hakuna sababu ya watu wengine kutamani kiti hicho kwa sababu wakiingia katika uchaguzi, wataangushwa na Sitta.

“Kwanza niseme kuwa mimi Lissu kwa mtazamo wangu binafsi, nakubaliana na uamuzi wa mzee yule (Sitta), hakuna mtu wa kuliweza Bunge hili zaidi yake na kwa vyovyote vile, mambo yatakuwa mazuri mbele yake,” alisema Lissu.

Alisema katika kipindi ambacho aliongoza Bunge la Tisa, watu wote walimkubali na kuamini kuwa angeweza kuwa kiongozi bora wa Bunge la sasa, lenye changamoto kubwa.

·

No comments:

Post a Comment